KUWA
NA USHIRIKA KAMA MTENDE
“Miti
ya Mitende huwa pamoja katika kundi na
hufanya chemchemi jangwani na kutoa kivuli kinachofaidisha viumbe vingine”.
M
|
iti
ya mitende ina sifa ya kuwa pamoja,Miti mmoja wa mtende ukiwa pekee yake
hauwezi kutoa kivuli cha kutosha na kujikinga na jua kali la jangwani. Kundi la
miti ya Mitende iliyo pamoja hufanya
chemichemi Jangwani.(Oasis).Mara nyingi mitende huwa pamajo na Kundi la mti ya
mitendi hufanya chemichemi inayofaidisha miti mingine tofauti nayo.
KWELI
YA KIROHO
Kama
vile ambavyo miti ya mitende ilivyo na tabia ya kukaa pamoja na kufanyika
baraka,Kadharika wenye haki nao wanapaswa kuwa na umoja na ushirika kati yao ambao
utakuwa chemichemi ya Baraka kwao na kwa
watu wengine.
Baraka Za Kuwa Katika pamoja katika Ushirika
Kutoka
kwa Mtende tunajifunza vile ambavyo wenye
haki wanaweza kustawi kwa kukaa na
kusimama pamoja. Agano jipya linafundisha umuhimu wa Waamini ambao ndio “wenye haki” katika Kristo kuwa na
ushirika na kukaa pamoja. Kuna faida nyingi sana za kukaa na kusimama pamoja
kwa wenye haki.Hapa ni baadhi
- 1.Katika Ushirika Tunafanyika Baraka Kwa Wengine
Mitende
inapokuwa pamoja kwa wingi mahali hutengeneza
chemichemi ambayo huitwa Oasis
.Lakini pia kuwa pamoja kwa miti ya mitende hutoa kivuli amabacho pia husaidia
wasafiri wanaochoka jangwani na wakaweza kupumzika na joto kali la jangwani.
Tunajifunza
kuwa ushirika wa wenye haki unaweza kuwa baraka sio kwao tu bali hata kwa watu wengine.Wanaweza kufanyika
faraja na masaada kwa watu wengi katika jamii.Umoja na ushirika wao unaweza
kuigusa jamii inayowazunguka kiroho na
kimwili.
- 2.Katika Ushirika Walio Dhaifu Wanainuliwa.
Mara
nyingi jangwani unaweza kuikuta miti ya machungwa na malimau yaliyokua chini ya
vivuli vya mitende.Hapa tunajifunza vile ambavyo wenye haki wanapokuwa pamoja
kama kundi katika kanisa wanatoa kivuli na kuwafunika wale waliodhaifu kuliko
wao.Ndio maana ni muhimu kuwa pamoja.
Paulo anafundisha
hivyo katika Warumi 15:1-2 Kwa kusema, “Sisi
tulio na nguvu, hatuna budi kuchukuliana na kushindwa kwa wale waliodhaifu wala sikujipendeza nafsi
zetu wenyewe.Kila mmoja wetu inampasa kumpendeza jirani yake kwa mambo mema,”
Maandiko
katika Waebrani 10:24-25,
yanatufundisha hivi, “Tuangaliane na
kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutendamema. Wala tusiache
kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi ya kukutana, tuhimizane sisi
kwa sisi kadri tuonavyo siku ile inakaribia.”
- 3.Katika Ushirika Hatuwi Kikwazo Kwa Wengine
Mti
wa mtende unanazo tabia zinazofaa kwa
mwenye haki.Katika miti yote ya pori mti wa mtende ndio unaotoa kivuli kidogo
zaidi.Kivuli chake hakiingili ukuaji wa mti mingine jirani yake na kuwa kikwazo
cha kupata mvua na mwangaza wa jua.Vivyo hivyo watu wa Bwana ,wenye haki hawazui
ukuaji na mafanikio ya wengine kwa kuwazuia mvua ya kweli na utukufu wa
mwangaza Mungu kuwaangukia wao.Wanafanya kila wawezalo kuwasaidia wengine
kushiriki Baraka za maisha.
- 4. Katika Ushirika Tunajenga Mahusiano Ya Kiroho Na Wengine.
Wenye haki
wanahitaji mahusiano ili kukua. Hatuwezi kukua nje ya wengine. Tunakua katika
dhana ya ushirika. Jambo hili tunalikuta tena na tena katika Agano Jipya. (Waebrania10:24-25)
Kukua
kiroho si suala binafsi na kipekee lina hitaji mahusiano na ushirika na wengine.Mafundisho ya kiroho
yanakuwa yanalenga umimi nakulenga mtu binafsi bila kulenga mahusiano yetu na
wengine si ya kibiblia na yanadharau sehemu kubwa ya Agano Jipya.
Mungu ametukusudia sisi tukue katika familia.
mawasiliano ni “gundi” ambayo inawaunganisha watu waaminio. Lakini pia
mahusiano hufanya kazi nyingine ya muhimu zaidi ya kuwasogeza watu katika
kukomaa .
- 5.Katika Ushirika Tunatimiza Amri Ya Kristo Ya Kupendana
Mahusiano ni
muhimu sana kwaajili ya kukua kiroho. Biblia hufundisha kwamba ushirika sio
suala la uchaguzi kwa Mwenye haki. Ni suala la amri. Wenye haki ambao
hawaunganiki katika mahusiano ya upendo na waamini wengine wanavunja “amri
nyingine” ambayo imetolewa na Neno la Mungu.
Yohana anatuambia kwamba uthibitisho ya kuwa
tunatembea nuruni ni kule“kushirikiana
sisi kwa sisi” (1Yohana 1:7) kama huna ushirika wa mara kwa mara na waumini
wenzako ni lazima ujiulize kwa umakini kama kweli unatembea nuruni au
vipi.Yohana anaendelea kusema kuwa tunalazimika kujiuliza kama kweli tumeokoka
ikiwa hatuwapendi waumini wengine.
1Yohana 3:14
“Sisi
tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda
ndugu yeye asiyependa akaa katika mauti”
Kiwango cha upendo wetu kwa Kristo unaweza kuonekana
katika kiwango cha upendo wetu kwa waumini wenzetu.Yohana anasema hivi, “Kwa kuwa mtu asiyempenda jirani yake, ambaye
Amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona ”(1Yoh 4:20).
Tambua kwamba
Yohana anasema “Hawezi”. Haiwezekani kumpenda Mungu kama huwapendi watoto
wake.Yesu pia alifundisha kwamba kama uko nje ya ushirika na ndugu yako, ibada
yako haina thamani. Mkristo hawezi kuwa na ushirika na Mungu na wakati huohuo
akawa hana ushirika na waamini wengine.
Meinrald Anthony Mtitu.
No comments:
Post a Comment