Thursday, July 13, 2017

SHERIA ZA KUPANDA NA KUVUNA-1


SHERIZA ZA KUPANDA NA KUVUNA-1

Kuna sheria ambazo unaweza kuishi bila ya kuzijua zipo zinafanya kazi.Kuna baadhi ya sheria za msingi za asili unapozipuuza ni hatari kwako  mwenyewe na ni kujileta madhara na uharibifu katika maisha yako. Moja ya sheria hizo ni hii  sheria ya kupanda na kuvuna.Msemo utavuna ulichopanda ni umezoeleka masikioni mwa wengi wetu lakini sio wote tunaoelewa kwa kina nini maana ya kanuni hii ya kimungu katika maisha yetu.




Kupanda na kuvuna ni sheria,kama vile ilivyo sheria ya uvutano na sheria nyinginezo.Sheria ya uvutano mara zote inafanya kazi kwa njia ile ile na kwa mtu yeyote yule,haichagui.Ndivyo ilivyo sheria ya kupanda na kuvuna.Ni kanuni ya kudumu isiyobadilika iliyo thabiti ambayo Mungu ameitengeneza katika uumbaji wake.
Sheria ya kupanda na kuvuna inaitwa sheria kwa sababu,Ni kanuni ya kimungu na sehemu ya ya Agano aliloliweka na Adamu na Uumbaji wote. Mpaka sasa nchi bado haijakoma,hii inamanisha kwamba kanuni ya kupanda na kuvuna inatendelea kuwa katika utendaji na watu wote wanajabika nayo.

Kila tunapotii sheria ya Mungu mwanzoni inahitaji Nidhamu na Imani lakini baadaye Baraka hufuatia.Na pale watu wanaposhindwa kumtii Mungu matendo yao yanakuwa hayana imani na mara nyingi huishia kujifunza kwa njia ngumu.

  1. Kupanda na kuvuna ni Sheria katika Ulimwengu wa Kilimo
Kupanda na kuvuna ni maneno  au msamiati ya kilimo.Wakulima  katika kipindi chote cha historia ya kilimo wameitegemea sheria hii  na imekuwa kweli katika ulimwengu wa kawaida na Neno la Mungu linasema kile kilicho kweli katika Kilimo ni kweli pia katika maisha ya yetu.
Katika kitabu cha Mwanzo  ambacho kina maanisha mianzo,tunaona udhihirisho wa kanuni ya mbegu ambayo inaendelea katika maandiko yote,na kanuni hii itadumu kadiri Nchi idumupo.


Mwanzo 8: 22 inasema hivi,
 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.”


Kama ilivyo katika kilimo kile  mtu apandacho katika maisha haya hatimaye atakivuna,sio kwasaababu labda Mungu atafanya kitu fula kisicho cha kawaida kukufany kitokee,bali ni kwasababu  hii ni kanuni ambayo ameiweka na hautewezi kutumia ujanja wowote ule uibadilisha.Hivyo usidanganyike na kufikiria unaweza kupanda mbegu mbaya na ukapona na kuwa salama.

Katika Wagalatia 6:7,Tunaambia na Paulo hivi, 

kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna

2.Kupanda na kuvuna ni Sheria katika Maisha ya kila siku
 Kanuni hizi za Kupanda na kuvuna zinatekelezeka au kufanya kazi kwa kila mtu, kwa wote Wakristo na wasio Wakristo.Hizi ni kanuni zisizo badilika,hakuna awezaye kuzikwepa,iwe ni kwa mwamini au asiye mwamini.Hizi ni sheria ya maisha. Kadiri nchi idumupo hakuna mtu atamdhihaki Mungu kwa kubadilisha hata mara moja tu hizi sheria za mavuno.
Maisha yamejaa na uchaguzi.Uchaguzi ambao unatuathiri sisi kila siku katika mambo tunayofanya.Hii inamaanisha uchaguzi wetu na maamuzi yetu ya kila siku hajapita bila ya  umuhimu wowote.Uchaguzi  wetu na maamuzi yetu yana tuathiri sisi na wengine katika njia ya kuvutia ambazo tunaweza tuzione mara moja au tusizone kabisa.
 “Sheria hii ya kupanda na kuvuna inafanya kazi kwa kila mtu na wakati wote,kwa mambo mazuri na kwa mambo mabaya
Sheria hii ya kupanda na kuvuna inafanya kazi kwa kila mtu na wakati wote,kwa mambo mazuri na kwa mambo mabaya.Hatuwezi kuikimbia na kuikwepa,au kuizunguka sheria hii.Mungu aliyeiweka sheria hii haidhihakiwi.Hivyo ni kusema maisha yetu leo ni matokeo ya mbegu ambazo tumezipanda jana.
Sheria za kuvuna na kupanda zinafundisha kila tendo katika maisha lina matokeo yake.Kile sheria hizi zinatufundisha ni kwamba, Kuna matokeo kwa kila matendo yetu mazuri au mabaya.Ulimwengu unatenda kazi  chini ya sheria ya chanzo na matokeo.Kwa kila matokeo tunayo yaona kuna chanzo chake au kisababisho chake. Hakuna namna ya kukwepa,Kila wakati tunapochagua matendo fulani ,basi tuna kuwa tumechagua na matokeo ya matendo hayo.

Kimsingi,hii inamaanisha kwamba kila tendo lina matokeo yake yanayoweza kutabiriwa.Kama nitapanda mahidi,nitapata mahindi,na sio viazi.Kama nitapanda tangawizi,nitapata tangawizi na sio ufuta.Kama nitapanda maharage,nitapata maharage na sio matikiti maji.Kadharika kanuni hii inafanya kazi kwa namna hiyo hiyo katika Ulimwengu wa roho.
3.Sheria ya kupanda na kuvuna ni kanuni ya kibiblia iliyo hakikishwa.
 Japo watu wengi kutokana na msisitizo ulipitiliza katika mafundisho ya kupanda na kuvuna yanayojikita kwenye sadaka pekee yake  wameichukulia kanuni hii kirahisi na kuiona labda sio ya kibiblia.Huu ni ukosefu wa uwiano katika kuifundisha kanuni Hii.
Ukipanda kukosoa  na kulaumu  katika maisha ,utarajie kuvuna kukosolewa na kulaumiwa na watu wengine katika maisha yako.Kama ukipanda utu wema ,utakwenda kuvuna utu wema,watu wengine watakutendea mema,sio lazima wawe ni wale wale ulio watendea mema wewe.

Sheria ya kupanda na kuvuna kunatumika kama  mfano wa kifo na mauti.Paulo alijadili juu ya fundisho la ufufuo wa mwili,alitumia mfano wa kupanda mbegu kuelezea kifo cha kimwili. I Wakoritho 15;42-22.Mbegu inaweza  “kufa’ pale inapoanguka aridhini,lakini sio mwisho wa maisha yake. Yohana 12:24

Inaendelea...
Meinrald Mtitu.



No comments:

Post a Comment

KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI

Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea...