Ewe Mvivu ,Utalala mpaka Lini?
Mithali 6:9-10
Ewe mvivu, utalala hata
lini? utaamka lini kutoka katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia
kidogo, bado kukunja mikono upate usingizi!Hivyo umaskini wako huja kama
mnyang’anyi na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Kitabu cha Mithali
ndicho ambacho kimezungumza sana juu ya uvivu kuliko kitabu kingine chochote
katika Biblia, kimetumia kwa wastani wa mistari 32 kuelezea namna ambavyo
uvivu haufai. Kitabu cha Mithali kina mahusia mengi ya maisha
hasa kwa vijana. Kitabu hiki kinazungumzia mithali za hekima, kuwafundisha
watu jinsi ya kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Mfalme
Sulemani ana uona uvivu ni kama moja ya hatari inayo wakabili watu
wengi hasa vijana.
Katika Fizikia kuna sheria ya kwanza ya mwenendo iliyovumbuliwa na Mwanasayansi aitwaje Isaack Newton,Sheria hii ya mwenendo inasema kwamba ikiwa kitu kipo katika mwenendo huelekea kubaki katika mwendo,na ikiwa kitu kipo katika mapumziko huendelea kubaki katika mapumziko.Sheria hii inatumika kwa watu pia.
Katika maisha ya kila siku kuna baadhi ya watu wanasukumwa kwa kawaida kuendea kufanya kazi au shughuli na kukamilisha miradi fulani,na wengine ni watu wanao wanahitaji motisha ili kuondoka na kwenda kufanya kitu,vinginevyo watabakia hapo hapo bila kufanya kitu chochote cha kuzalisha.Hili kundi la pili ndilo la watu wanaitwa wavivu
Katika maisha ya kila siku kuna baadhi ya watu wanasukumwa kwa kawaida kuendea kufanya kazi au shughuli na kukamilisha miradi fulani,na wengine ni watu wanao wanahitaji motisha ili kuondoka na kwenda kufanya kitu,vinginevyo watabakia hapo hapo bila kufanya kitu chochote cha kuzalisha.Hili kundi la pili ndilo la watu wanaitwa wavivu
UVIVU NI NINI?
- Uvivu ni mlango wa dhambi nyingine kupata nafasi kuingia katika maisha ya mtu.
- Uvivu ni shauku ya kuwa bure bila kazi au shughuli yeyote.Ni Kutulia tu.
- Uvivu ni kuwa mlegevu na mzembe katika kufanya mambo.
- Uvivu ni ile hali ya kutofanya chochote na kutofanya juhudi zozote za kufanya kitu.
- Uvivu ni hali ya kukaa tu na kuacha mambo yakae na kubakia kama yaliyo.
- Uvivu si chochote zaidi ya tabia ya kumpumzi kabla hatujachoka - Jules Renard
- Mtu ambaye hamalizi majukumu yake kwa wakati ni mvivu.
- Mtu ambaye haonekani kwenye kazi yake kwa muda wa kazi huyo ni mvivu.
- Mtu ambaye anakwepa majukumu yake ya kazi huyo ni mvivu.
- Mtu ambaye hawezi kuanza na kuendeleza jambo fulani lililo katika uwezo wake ni mvivu.
- Uvivu ni uhairishaji wa shughuli ambao hauwezi kuutawala tena.
ONYO KWA WAVIVU WOTE.
Mtume Paulo
naye alikemea kwa nguvu juu ya uvivu miongoni mwa waamini katika Kanisa
la Wathesalonike.Na yeye mwenyewe alikuwa ni mfano kwao wa kufanya kazi kwa
bidii.
2 WATHESALONIKE 3:6-9
Ndugu, tunawaagiza
katika Jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na
ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa. Maana ninyi wenyewe mnajua jinsi
iwapasavyo kufuata mfano wetu.
Sisi
hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, wala hatukula chakula
cha mtu ye yote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku
na mchana, ili tusimlemee mtu ye yote miongoni mwenu.
Tulifanya hivi, si kwa
sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, lakini ili kusudi tujifanye
sisi wenyewe kuwa kielelezo.” Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa
amri ili kwamba: ‘‘Mtu ye yote asiyetaka kufanya kazi, wala asile.’’
1 WATHESALONIKE 4:11-12
Jitahidini kuishi maisha
ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi
kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza, ili maisha yenu ya kila siku yajipatie
heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu ye yote
AINA NNE (4) ZA
UVIVU ZILIZOFICHIKA
Kwa kawaida huwa
tunachukulia uvivu kwa vile vitu ambavyo ni rahisi kuonekana.Kwa uelewa huu wa
uvivu umetufanya tuamini kama tunaonekana kwenye kazi zetu na kuzimaliza basi
sisi sio wavivu. Kitu ambacho sio kweli.Kuna aina nyingine
nyingi za uvivu ambazo huenda unazitumia kila siku na zinaendelea kukurudisha
nyuma. Huwezi kufikia mafanikio makubwa kama utaendelea na hizi aina nyingine
nyingi za uvivu. Hebu angalia aina hizi ya uvivu.
Uvivu wa kutoyafanya yale uliyoyapanga kufanya.
Kitendo cha kupanga wewe
mwenyewe kwenye nafsi yako kwamba utafanya kitu halafu usifanye ni uvivu. Kwa
sababu kwa akili zako timamu ulikubali kwamba kuna kitu utafanya au kubadili
kwenye maisha yako, sasa mbona hufanyi kitu hicho?
Ulisema utawahi
kuamka, mbona hufanyi hivyo? Ulisema utaanza kuweka akiba, mbona
hufanyi hivyo? Ulisema utaacha kupoteza muda mbona hufanyi hivyo? na mambo
mengi kama hayo. Huo pia ni uvivu uliojificha.
Uvivu wa kutofikiri juu ya maisha yako mwenyewe.
Moja ya uvivu
uliojificha ni uvivu wa kufikiri.Watu wengi ni wavivu katika
eneo hili.Eneo hili lina wavivu wengi sana,watu wengi ni wavivu
kufikiri ni nini wafanye,wako radhi kufanya mambo mengine yote lakini siyo
kufikiri.Kufikiri ni kazi ngumu sana kwa watu wavivu.
Kusubiri watu wafikirie
kwa niaba yako kwamba uishi vipi nao ni uvivu mkubwa sana. Kama huna mipango na
maisha yako na unafanya kile ambacho kila mtu anafanya, basi wewe ni mvivu.
Hakuna kundi jingine tunaloweza kukuweka. Kwa nini usikae chini na kuamua ni
maisha gani unayotaka kuishi wewe, kwa nini utake tu kwenda kama hujui unakoelekea?
Uvivu wa kutofanya mambo kwasababu
ya kuogopa na kutokuwa na uhakika.
Kuogopa kufanya jambo
kwa sababu huna uhakika au ni jambo jipya nao ni aina ya uvivu
uliojificha.Ndio, uvivu unakufanya uone ni kitu ambacho hakiwezekani kufanyika.
Kama ukiondokana na uvivu na kuweza kufanya huenda ukaleta mabadiliko makubwa
sana.
Uvivu wa kuahirisha mambo ambayo ulipaswa
kuyafanya.
Kuahirisha mambo nao ni
uvivu tena mkubwa sana. Yaani kwa nini upange mwenyewe kwamba muda fulani
utafanya kitu fulani, halafu wewe mwenyewe useme hutafanya tena, tena bila
sababu ya msingi? Huu nao ni uvivu uliojificha.
Uvivu wa kukwepa kufuta njia ndefu ya kufikia
kwenye mafanikio.
Kutafuta njia ya mkato
hasa kwenye kufikia mafanikio nao ni uvivu mkubwa sana. Na mara zote
unaposhawishika kupita tu njia ya mkato ili upate mafanikio ni lazima upotee.
No comments:
Post a Comment