Usikate Tamaa,Mungu Atayafuta
Machozi Yako.
Katika
maisha haya kuna nyakati tunalazimika kupitiza vipindi vya machozi na nyakati za kupoteza na hasara.Baada
ya kupoteza jambo Fulani ambalo tulikuwa tumeambatanishwa nalo kwa kina huwa
tunapitia katika nyakati za huzuni na maombolezo.Kupoteza,hasara ni sehemu ya
maisha yetu mafupi na vi vema tujue jinsi ya kukabili hali hii inapotupiga.
Wakati
kitu Fulani au mtu mfulani ambaye tulimpenda na kumfurahia anapoondolewa, maisha
yetu hupaki katika machafuko na mvurugiko. Habari njema ni kwamba bado kuna
maisha tena na bado kuna uhai tena hata baada ya kupoteza.
Kupoteza
haimaanishi ni mwisho wa kuishi,Wakati mwingine hatuwezi kujifunza kwa njia
yoyote ile.Hulazimu tupoteze kwanza ndipo tuweze kujifunza.Kupoteza na hasara huja
na somo la thamani ambalo hatuwezi kujifunza kwenye shule yoyote.
Kama watu wa Mungu tunapaswa kuachilia Maumivu na huzuni zetu na kuendelea mbele hata
baada ya kupoteza na hasara katika maisha yetu kwani Mungu bado ana mpango juu
ya maisha yetu na atatutokea kwa njia nyingine na kutuhuisha tena.
Baada Ya Kupoteza Usiendelee
Kuishi Katika Hali Ya Maombolezo Na Huzuni.
Ukisoma katika [MWANZO 35:16-21]
Yakobo alimpenda sana Raheli ,alimfanyia kazi miaka 14 kumpata.Raheli alipofariki wakati wa kuzaa kwake, Yakobo alimpoteza mpenzi wa maisha yake alibaki mpweke kwa na mtoto mchanga Benjamini wa kumlea mwenyewe.Pamoja na hayo yote Biblia inatuambia aliendelea mbele. ,Yakobo alijenga nguzo wa ukumbusho na kuendelea mbele.

Kuna
wakati watu wale tunaowapenda katika mazingira tofauti wanaondolewa
kwetu,wakati mwingine tumewekeza sana katika mahusiano halafu hajafaulu,wakati
mwingine ni kazi tuliyofanya na kuijenga kwa bidii halafu inapotea.Wakati mwingine ni juhudi zote tulizoweka katika kuyajenga maisha yetu zinapoteza.Au ni biashara tuliyowekeza fedha zetu nyingi na muda inafeli.n.k.
kama wanadamu tuna tengeneza nguzo za maombolezo na huzuni ,lakini hatupaswi kuishi chini ya nguzo hizo daima.Tunatakiwa kuendele mbele kama Yakobo.Watu wanao endelea mbele wanajua kuna siku bora mbeleni na Baraka kubwa usoni na sio katika siku zilizopita.

Pamoja na hasara
na kupoteza kwako uone Mungu bado anatenda kazi katika maeneo na hali
nisiyoweza kuyaona:
[MWANZO 37:34-35].Baada ya kifo cha Raheli,Yakobo
alihamishia upendo wake wote kwa Yusufu
na akampenda sana kuliko kaka zake na jambo hilo likaleta uadui kati yao hata
waka muuza utumwani Misri na kumdanganya
Baba yao kuwa ameuawa na mnyama makali.Yakobo alifadhaika sana na kuomboleza na
kukataa kufarijiwa..
Sikia mtu wa Mungu,Usikate tamaa wala kuacha kuendelea kwasababu ya hayo magumu yaliyokukuta, kwasababu pamoja na hasara zetu na kupoteza kwetu,Mungu bado anatenda kazi katika maeneo ambayo hatuwezi kuona.Mungu anayo sababu ingawa hatuwezi kuelewa sasa,siku moja tutaangalia nyuma na kutikisa kichwa na kukubaliana na Mapenzi ya Mungu.
Usione hali yako ya kupoteza ni kama ni ya kudumu,ni ya kitambo tu na siku moja Mungu ataleta vipande vya maisha yako pamoja na utafurahi na kushangaa kazi ya mikono yake.
[MWANZO 42:1-36]
Hatimaye njaa inatokea Kanani na Yakobo anawatuma watoto wake 10 Misri kununua chakula ,wanakutana na Yusufu yeye anawatambua na kuwajaribu,Simeoni anafungwa na wengi wanaashiwa kwa sharti la kumelea Benjami.Yakobo anaposikia haya anachanganyikiwa zaidi analia na anaomboleza.Anapitia kipindi kigumu zaidi cha maisha yake Yakobo anahesabi hasara zake ,yale aliyopoteza,hata anawaza amelaaniwa,anaona amepoteza mara nyingi zaidi,na mbaya zaidi hata Benjamini wanataka kumchukua.

Tazama,Kuna wakati kila kitu kinaonekana
kipo kinyume nasi,hasara inaongezeka,maadui wanaongezeka,marafiki
wanatuacha,watu tuliowaamini na kuwategemea wanatudanganya,tunateseka kwa kutotendewa haki,mahusiano yanavunjika, ndoa ina inavunjika, watoto wetu wana tuasi,biashara
ina feli,Inaonekana kama kuzimu yote imeashiliwa kutushambulia na tumefika
mwisho wa kamba na mwisho wa njia.
Wakati umefika mwisho wa kamba yako usipoteze matumaini kwa sababu Mungu atakupa neema ya kuenenda nayo hiyo hali.Kila kitu kinaweza kuoneka kipo kinyume nawe lakini Mungu yupo kwaajili yako na unaweza usimwone au usimhisi lakini anatenda kazi nyuma ya pazia kwa niaba yako na siku moja atafungua pazia na utaona matendo makuu aliyoandaa kwaajili yako.

Kukubali
kuachilia vile vitu vizuri kwako ili Mungu akupe vilivyo bora zaidi
Njaa ilipo endelea sana Kaanani
walihitaji chakula lakini sharti la Mfalme Joseph lilikuwa,ni lazima Benjamini
aachilewe ,apelekwe ili wapate chakula na wamuone Simioni tena.Haikuwa rahisi
kwa Yakobo kumwachia Benjamini kwenda.Benjamini ilikuwa ni kila kitu
kwake,alikuwa amaeungamanishwa naye sana.Benjaminini faraja yake ya mwisho, alikuwa anamkumbusha
Raheli,na Yusufu.Hivyo kitendo cha kumwachia aende ilikuwa na vita.
Hatuwezi kuona nini Mungu ametuwekea
mbele yetu mpaka tuwe tayari kuachilia yaliyopita.Tunapoyaachilia tunatengeneza
nafasi kubwa kwaajili ya Baraka bora zaidi.Katika maisha yetu kuna vitu huwa
vinapotea lakini huwa vina rudishwa kwa utukufu mkubwa zaidi kuliko
mwanzo.
Wakati Yakobo hataki kumwshia Benjamini kwa hofu ya kupoteza zaidi,Mungu alikuwa ni kama anamwambia Mzee yako ukitaka kuona maajaabu niliyo kuandalia kwa miaka hii yote,mwachie Benjamini aende.Kuna wakati wa yule Yusufu wetu aliyepotea kurudi kwa utukufu sana,lakini kwa gharama ya kumwashia Benjamini wetu tunaye mlinda sana.
Wakati mwingine tunahitajika kuachilia vitu vizuri amabavyo ni vya thamani kwetu lakini kama tutaviachilia vile vizuri,Mungu hutupa vilivyo Bora na kama tukiviachilia vilivyo Bora,hutupa vilivyo Bora Zaidi.Usisubiri Mpaka Mungu akuvunje mkono wako ndipo uachilie.
Sikia,Kadiri unavyochelewa kumwachilia Benjamini wako,ndivyo unavyo chelewesha kukutana kwako na Yusufu wako.Wakati mwingine siri ya kufanikiwa ni kutenganishwa ,na kutenganishwa ni maumivu.Haijalishi nini ,kama Mungu amesema achilia kiende,basi inamaanisha Mungu ana kitu au jambo bora zaidi mbeleni.

Mungu
hufuta machozi na maumivu yetu ya kupoteza kwa urejesho na kutuhuisha tena.
MWANZO 45:26-28
Wakatoka Misri, wakafika nchi ya Kanaani kwa Yakobo, baba yao. Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadikiWakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka. Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla sijafa.
Maisha ya Yakobo yalijaa taarifa mbaya lakini hatimaye alikuwa sasa anasubiri kusikia taarifa njema ambayo hataweza kuistahimili na itafuta machozi ya hasara na maumivu yake.Habari njema itabadilisha maisha yake daima na habari ilikuwa ni Yusufu yu hai,hajafa.Baada ya hasara zote na kupoteza kote hatimaye ikwa ni wakati wa Yakobo kupata na kupokea.
Mpendwa,Mungu huleta urejesho,habari njema zitatujia, yasiyowezeka yatatokea katika maisha yetu.Mungu ataenda kuwaabisha maadui zako.Na kile ulichopata hasara na kukipoteza kinakwenda kurudi kwa namana kuu.Mungu wetu ni Mungu wa Urejesho.

Adui amekuvunja moyo kwa mambo mengi
lakini Mungu atatenda jambo moja ambalo litabadilisha kabisa maisha yako. Umepoteza,umeomboleza,umelia,lakini
Mungu anakwenda kugeuza maombolezo yako kuwa machezo,machozi yako kuwa
kicheko,huzuni yako kuwa wimbo mpya,majivu yako kuwa uzuri na hasara yako kuwa
faida.
Nini
umepoteza,nini unaomboleza na kulia kwaajili ya hicho usiku na mchana,ni wakati
wa kujenga nguzo ya ukumbusho na kuendelea mbele.Kumbuka Mungu yupo anatenda
kazi hata sasa nyuma ya pazia.Pengine unahitaji kumwachia Benjamin wako tumaini
lako la mwisho ili umpate Yusufu wako aliyekuwa “amekufa”.
Meinrald Mtitu
Light of Hope Teaching Ministires
Meinrald Mtitu
Light of Hope Teaching Ministires
No comments:
Post a Comment