Wednesday, June 28, 2017

KUWA MSHINDI KAMA MTENDE

KUWA  MSHINDI KAMA MTENDE

“Matawi ya mti wa  mitende hutumika kama ni Alama ya ushindi      na furaha”

ZABURI 92:12-13
Mwenye haki atasitawi kama mtende, Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.

    M
tende ni mti unaobeba alama ya mafanikio na ushindi. Kwa miaka mingi matawi yake yametumika kuonyesha alama ya ushindi furaha na Amani.Mara nyingi katika Neno la Mungu kila mahali matawi ya mitende yalipo tumika yalihusianishwa na ushindi.
 Mfano Kwenye hekalu la Sulemani Tunaona mitende ilikuwa ni moja ya michoro iliyokuwepo kwenye hekalu la Sulemani ikiashiria ushindi.Matawi ya Mitende tunaona yakitumika kumshangilia na kumwimbia Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu.

YOHANA 12:12-13

Siku iliyofuata umati mkubwa uolikuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana! Amebarikiwa Yeye ajaye kwa Jina la Bwana! Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!’’

Katika Kitabu cha UFUNUO 7:9-10 tunaiyona mitende ikitajwa na ikieleza vile Watakatifu  walio vaa mavazi meupe wakiimba kwa ushindi mkuu wakiwa wameshika matawi ya mitendi mikononi mwao  wakiashiria Ushindi.

“Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;”

KWELI YA KIROHO:
Mungu anawafananisha wenye haki na miti ya mitende kwasababu anawataka wawe na maisha ya Ushindi.Wenye haki ni washindi ndani ya Kristo.Ndani ya Kristo Wanashinda na zaidi ya kushinda.

Biblia inatumia majina mengi kuwaelezea wale walio ingia katika maisha  ya uhusiano binafsi na Bwana Yesu Kristo,moja ya majina hayo wanaitwa ni Washindi.Hiki ni cheo ambacho Yohana anakitumia katika nyaraka zake.

 I Yohana 5:4
Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kuushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu”

Mtume Paulo naye anawaeleza wale walio mwamini Kristo kama ni watu walio washindi na wenye ushindi katika mambo yote.

WARUMI 8:37
Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda

Mshindi Ni Nani ?

Mshindi kwa kiingereza overcomer katika maana ya kawaida  ya lugha ya kiyunani “nikao” ni victor, pia tunapata neno nike. Ambalo  wayunani walilitumia kama jina la mungu mke wa Ushindi. Katika Imani zao waliamini ushindi unapatikana kwa miungu tu na sio wanadamu,miungu tu ndio ilikuwa washindi na walikuwa hawashindwi.

Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kuushinda kuushindako                           ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.-       
Mtume Yohana,” 100 A.

Sisi tu washindi wa wokovu,ni wale tu waliozaliwa na Mungu ndio washindi wa kweli.Ushindi wetu ni kwasababu tu tupo ndani ya Kristo aliye mshindi.Yesu alitumia neno hili nikao katika Yohana 16:33 pale aliposema kwa maana Mimi nimeushinda ulimwengu.’’ Ni neno Mshindi.Yesu alikuwa anasema kwamba ameushinda mfumo wa Shetani.


Ukweli kuhusu maisha ya Mkristo ni kwamba yupo ndani ya Kristo,hawezi kutenganishwa katika Muungano wake na Kristo mwenyewe hivyo yu mshiriki wa asili ya uungu.Mkristo anashiriki kila kitu alicho nacho Kristo, Hii ni pamoja na urithi,haki,mauti,uzima na Roho.Kwa vile Kristo ni mshindi  na Mwamini pia ni Mshindi.Wale walio zaliwa na Mungu ndio washindi wa kweli.

No comments:

Post a Comment

KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI

Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea...