USIKATE TAMAA,MUUJIZA WAKO UPO
KARIBU
Mara nyingi
tunapokutana na changamoto za maisha huwa mapema sana tuna simama na kuacha
kuendelea mbele.Tunakata tamaa mapema mno, tunavunjika moyo mapema mno,tuna
salimu amri mapema mno kwa mazingira na hali yetu wakati kumbe Muujiza na
ushindi wetu upo karibu tu mbele yetu.
Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili
na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji.
Wana wa Israeli baada ya kutoka
Mara mahali palipo kuwa na maji machungu
na waka vunjika moyo sana na kukata tamaa hatimaye wakafika mahali kwenye chemichemi za mitende
palipo itwa Elimu.Hapa palikuwa ni mahali pa muujiza wao baada ya kuwa katika hali
ngumu ya kukosa maji.
Elim hapa mahali palikuwa na
chemichemi kumi na mbili na mitende sabini.Ni mahali pa zuri pa kuwaburudisha baada
ya kupitia hali ya kukuakiwa na kiu ya maji.Hatimaye sasa wamefika Sinai ,katikati ya Jangwa na kuna raha ,kuna
chemichemi ,na kuna maji yote wanayohitaji.Huu ni muujiza mkubwa sana kwao.
Kuna swali la
kujiuliza kwani kuna umbali gani toka Elim mpaka Mara? Ukiangalia ramani ya
nchi takatifu na kuangalia ilipo Mara na
ilipo Elim,utaona ni kama Maili 5 tu sawa kilomita kama 8 tu.Yaani ni kuzunguka
tu kidogo kutoka walipokuwa Mara kwenye
maji machungu na tayari mbele kidogo kuna mahali pana maji tele.Lakini bado
walikuwa wana laumu,kulalamika , na kunungunika na walikuwa tayari kukataa
tamaa.
Kuna somo kubwa sana hapa katika maisha yetu ya kila siku.Hatu takiwa kukata tamaa mapema,kwani
wakati mwingine muujiza wetu unakuwa ni karibu mno kuliko tunavyofikiria. Kumbe
kuna wakati‘Elim yetu’ mahali ambapo
matumaini yapo ni maili tano tu mbele,ni
ni kuzunguka kidogo tu na kupafikia.Kwa kukataa tamaa na kusalimu amri tunaweza
kuukosa muujiza wetu ambao tulikuwa tumeukalibia sana.
Hii
inakumbusha hadhithi ya kweli
iliyotokea miaka kadhaa iliyopita pale
ndege ilipoanguka katika maeneo ya Andes, ambapo watu waliosalimika baada ya
kukaa kwa muda bila chakula waliamua
kuanza kulana nyama wao kwa wao na
kufa.Kumbe nyuma tu ya mlima ya Andes waliopokuwepo kulikuwa na kituo kikubwa cha mchezo wa kuteleza katika barafu
mahali ambapo wangeweza pata msaada na chakula.Kwa kuwa hawakufikiria kama wangeweza
kupata masaada na wakakata tamaa hivyo walikaa
kwenye ndege pale walipo na kuishia kulana na kufa.
Katika maisha haijalishi
tunakabiliwa na changamoto gani tusiwe wepesi
kukata tamaa.Mara nyingi ushindi katika michezo hupatikana katika
sekunde mbili au tatu za mwishoni.Elim
yako haiku mbali,mahali ambapo majibu
yako na matumaini yapo ni mbele tu kidogo.Mahali ambapo kuna mlango na mpenye wako
ni karibu kuliko unavyo fikiri,Usikate tamaa.Usiache endelea kusonga mbele lipo
tumaini.
Unawezaje
kufika Elim kutoka Mara? Unawezaje kutoka mahali pa kuvunjika moyo na kwenda
mahali pa matumaini na kufurahia? Kuna jibu moja tu.Kufika hapo endelea kwenda ,endelea kwenda mbele.Endelea
kumtumaini Mungu.Angalia maandiko hayasemi kwamba ni Mungu aliwaletea Elim pale
walipokuwa.Hakufanya hivyo ,wao ndio walio paswa kwenda mbele mpaka wafike
Elim.
Njia moja pekee
ya kutoka mahali pa kuvunjika moyo na
kwenda mahali pa matumaini na furaha ni kuendelea kwenda mbele tu.
Elimu ilikuwa
maili 5 tu mbele.Lakini walitakiwa kuifikia kwa kuendelea kwenda bila kujali
hisia zao,ingawa walikuwa na maumivu moyoni, ingawa walikuwa wamevunjika moyo
na kukata tamaa.Njia pekee ya kutoka Mara kwenda Elim ni kuendelea kwenda.Njia
pekee ya kutoka kwenye kuvunjika moyo na kukata tamaa na kwenda kwenye
furaha ni kuendelea kwenda.Endele kwenda mbele.
Kuna wakati
fulani hujisikia kuomba kabisa,hujisikia kuendelelea kutumaini,hujisikii kabisa
kutoa wala kutumika na pengine hujisikia kabisa hata kuabudu.Ufanyaje katika
hali hiyo,jibu ni endelea kuomba hata kama hujisikii,endelea kutumaini ,endelea kutumika,endelea kutoa hata kama
hujisikii,endelea kufanya yale unayoyafanya.Usiache na kukata tamaa na kufia
jangawani.
Kuna wakati husiki kabisa moyo wako upo kwenye
hilo jambo, Unapoteza moyo wako katika jambo hilo.Je,ufanyaje? Endele kwenda
mbele.Tunashushwa mioyo mara nyingi na mambo mbalimbali,lakini Neno la Mungu
linatuambia tusivunjike na kushushwa mioyo tuendelee mbele.
Pengine
hujisikii kuendelea na hiyo kazi unayoifanya na unatamani ubaki nyumbani tu na
kuangalia Tv. Au kulala tu siku nzima,Haijalishi unajisikiaje endelea na kazi. Nenda kazini usibaki nyumbani.
Ni watu wasiokomaa ndio wanao ishi kwa kufuata vile wanavyojisikia yaani hisia zao.Watu
waliokomaa wanaishi kwa kufuata kujitoa kwao kuliko hisia zao.Wanaendelea
kutumika ,sio kwasababu wanajisikia vizuri bali kwasababu kutumika ni jambo
jema kufanya.Na wanaendelea vema.
Meinrald A. Mtitu
No comments:
Post a Comment