Usikate
Tamaa ,Chagua Kubakia Na Matumaini
“Kukata tamaa kuna kula shimo katika mioyo yetu.Kunatufanya
tutamani kukimbia, na Kunajaribiwa kufanya mambo
ambayo hatupaswi kufanya”.
Kadiri unavyoishi miaka mingi utakubaliana nami
kwamba Maisha ni mchanganyiko wa maumivu na raha,ushindi na kushindwa,mafanikio
na kutofaulu,kuwa juu ya mlima na kuwa chini bondeni. Kama watu wengine
wote,Walio mwamini Yesu Kristo nao wanapita katika matatizo
mbalimbali maana nao bado wanaishi katika ulimwengu huu huu ulioanguka.
Wakristo wanavunjika moyo,Wanakata
tamaa,wanaugua ,Lakini pia wana matatizo ya kifamilia,matatzio ya kifedha n.k
kama watu wengine. Lakini kuna tofauti na tofauti hiyo ni kubwa.Wakati Wakristo
na wasio wakristo wanapitia katika changamoto zilezile za maisha ,tofauti ni
kwamba Wakristo wao wanalo tumaini kwamba Mungu yupo pamoja nao.Sisi
Tulio mwamini Yesu Kristo tuna uhakikisho kwamba kwa kadiri ambavyo Yesu yupo
nasi,sisi ni zaidi ya washindi.Yesu ni tumaini letu.Yeye ni zawadi ya Mungu ya
neema kwetu.
Kuwa na
Matumaini katika nyakati ngumu ni Uchaguzi ambao kila mtu anaweza
kuufanya
Kila mmoja anauwezo wa kuchagua kuwa na
matumaini.Inahitaji ujasiri kwasababu matumaini yanaweza kukuvunja moyo na
kukuangusha. Biblia inasema hivi katika Mithali. “Kile kitarajiwacho kikichelewa
Moyo/Nafsi huumia’.
Pamoja na hayo bado na shawishika kwamba ule
ujasiri wa kuchagua matumaini siku zote huwa unalipa.Ni bora mara elfu nyingi
kuchagua kuwa na matumaini kuliko kutokuwa na matumaini yeyote.
Kama umevunjika moyo ni kwa sababu ya uchaguzi wako,ni wewe
umeamua kuvunjika moyo, kwasababu kuvunjika moyo ni uchaguzi.Huna sababu ya
kuamua kuvunjika moyo,lakini ni wewe unayeamua kuchagua mawazo ya kuvunjika
moyo.
Ni wewe unachagua kuangalia hasi,ni wewe unaye chagua kuto mwangalia
Kristo na mambo yote mazuri,na unaangalia mabaya.Huu in uchaguzi na unaweza
kuubadilisha.Ndio maana ,Mungu anakutaka uchague kwa hiari na kutenda.
Unaweza kujiuliza Ninawaje kuchagua kutokuvunjika moyo? Ni
kwa kuweka mtazamo wako na kukaza kuangalia Katika Nguvu za Mungu
kuliko katika matatizo yako.Unaweza kuwachukua watu wawili na
kuwaweka katika hali inayofanana ya machafuko, mgogoro,na
ugumu.Lakini mmoja wao atapeperushwa na hali hiyo,wakati mwingine atafanya
imara,mwingine ataanguka, na mwingine ata imarishwa kupitia hali hiyo hiyo moja,
Tofauti ni wapi mkazo wa mtazamo wao
ulikuwa.Hupaswi kukaza kutazama mazingira yako,bali kukaza kumtazama
Kristo.Siyo kutazama hali yako,lakini kumtazama Mwokozi,siyo
Matatizo yako,lakini Nguvu za Mungu.
WAKOLOSAI 1:11
"Mungu akiwatia nguvu ninyi kwa Nguvu zake
mwenyewe ili kwamba msikate tamaa wakati matatizo yanapo wajia bali muwe na
saburi/uvumilivu.
Nguvu za kibinadamu huwa zinaisha.Baada ya
kupitia jaribu kwa muda fulani,unajikuta huna nguvu zilizobakia.Uvumulivu wa
kibinadamu una kikomo,huwa unafika mahali unaisha.Unapofika katika hali kama
hiyo hapo sasa unahitaji chanzo cha nguvu kilicho kikubwa kuliko wewe!
Unapokuwa katika kukata tamaa na vile
maisha yalivyo,Kama unafikiri utaweza kupita katika hali hiyo kwa nguvu zako
mwenyewe sahau,huwezi.Huna nguvu za kutosha kushughulika na mambo ambayo
utakumbana nayo katika maisha.Unahitaji kujichomeka kwenye chanzo cha
Nguvu kilicho kikubwa zaidi yako mawenyewe na chanzo hicho ni Mungu
mwenyewe.
No comments:
Post a Comment