Tuesday, July 11, 2017

KUWA THABITI KAMA MTENDE

KUWA THABITI  KAMA MTENDE


Mtende unatabia ya kupinda bila ya kuvunjika
ZABURI 92:12-13
Mwenye haki atasitawi kama mtende, Waliopandwa katika nyumbaya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu

M
oja ya tabia na mitende ni uwezo wakustahimili dhoruba kali ya jangwani bila kuathirika.Miti ya mitende ina sifa ya kipeeke inaweza kupinda lakini sio kuvunjika.Dhoruba inaweza kuupindisha mti wa mtende inavyotaka lakini ikisha pita tu mti wa mtende hurudi katika hali yake ya kuwa wima.

 Mti wa mtende unatabia nyingine yakutoweza kukandamizwa.Kama ukiweka jiwe nzito mahali pale  ambapo  kuna dalili   ya mti wa mtende kuchipua utashangaa.Baada ya muda  mti wa mtende  utaliinua jiwe au kupenyeza  kwa pembeni na kuendelea na kusudi lake na kwenda juu.

Kuna kisa ambacho mtu mmoja alisimulie vile ambavyo wakati mmoja aliishi kwenye nyumba ndogo  na mti wa mtende uliota na kupenye kwenye sakafu  bila kuzuiliwa na hatimaye ukatokea kwenye paa.

KWELI YAKIROHO  

Kama vile mtende ulivyo Imara katika dhiki ,kadharika Mwenye haki  naye anategemewa kusimama Imara katika majaribu  anayopitia maishani.

Maisha ya watu wa Mungu yana dhoruba nyingi za kuwapiga lakini wale waliostawahi vizuri kiroho huwa hawaondoshwi na dhoruba hizo, zinaweza kuwapindisha lakini sio kuwavunja. Kama vile mtende unavyo imarishwa  na dhoruba,kadharika Majiribu na adha haviwezi kumuathiri Mtu mwenye haki kinyume chake  vinamfanya  kuwa  thabiti na imara zaidi .

Wenye haki hawazuiwi na kukandamizwa kirahisi kutoka kwenye safari yao ya kwenda juu.Wanakataa kuzuiwa na magumu ya maisha haya.Wapo kama mtende, pale inaposhindikana kwao kuondoa vizuizi vilivyo katika njia yao, basi watavizunguka,watavivuka  na ikilazimu watapita katikati yavyo kwa kila namna ili wafike kule walikodhamiria kufika.

Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;  twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi; -   
Mtume Paulo

Namna ile unavyoyaitikia majaribu ya maisha kunafunua kwa kiasi kikubwa kuhusu nguvu   za imani yako katika Kikristo.Kama tukikana matatizo yetu au tukiyakasirikia au kuwa na uchungu au kama tukiwalaumu wengine kwa matatizo yetu,basi tunakosa kile Mungu alichokusudia kutufundisha sisi kupitia yale yanayotutokea.

Ni ukomavu wa kiroho kuwa na uwezo wa kuseme “ Naamini Mungu ameruhusu ugumu huu ninao pitia kwa faida yangu na kwa utukufu wake”

Mtazamo wa Mwenye haki juu ya taabu na   dhiki

Katika 2 Wakoritho 4: 8-9,  Paulo anazungumza mambo manne yanayoelezea namna gani Wenye haki tunavyoweza kutikia na kuyapokea majaribu katika maisha yetu.   Anasema , “Tumekandamizwa kwa nguvu kila upande,lakini hatukuvunjika, Tumefadhaishwa lakini hatukati tamaa ;tumeteswa,lakini hatuja telekezwa,Tumepigwa chini lakini hatuja haribiwa.”

  • Makandamizo na mbinyo wa matatizo havimshindi mtu mwenye haki.


Kubinywa kunakozungumzwa na Paulo   ni mfano wa vile zabibu zinavyo kamuliwa kwenye  chombo chake maalumu na kuzishinikiza zabibu. Paulo anachosema ni kwamba mashinikizo ya maisha yanaweza kuwaminya  wenye haki  lakini mwisho bado hawahi wemesagika na kupondeka.Katika uhalisia wa maisha tukiwa wenye hali wa Bwana, hatukandamizwi mara kwa mara lakini mara nyingi tutakandamizwa. Tunakandamizwa kila upande na matatizo kwa sura mbalimbali lakini hatusagiki.Kama mtende ,wenye haki tunapindwa lakini hatuvunjiki.

  • Machafuko Hayamvunji moyo mtu mwenye haki


Kama wenye haki kuna nyakati hatujui njia ipi twenda. Kuna wakati mambo yanakuwa ni magumu kwa wenye haki,maisha yana namna ya kuturushia mawe ambayo tunahangaika kuyakwepa.Kuna nyakati tunakabiliana na mazingira ambayo yanatuchanganya na kwa kweli hata hatujui nini tunahitaji au nini tunataka au kipi kitakuwa bora.Kuna nyakati hatujui hata tuombe vipi.

Paulo  mwenyewe analisema hili katika Warumi 8:26. Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” 

Kuna nyakati ambapo mbinyo na mkandamizo ,shinikizo unakuwa mkubwa sana na tuna kuwa tumechoka sana na kuchakaa na maisha yanakuwa yanachanganya na kiasi kwamba tunashindwa kujua nini tuseme na Bwana.Uchovu unatuchakaza kabisa,Sisi tunachanganyikiwa na kufadhaika,na wakati mwingine hatuna uhakika itakuwaje.Katika hali zote bado fadhaa hizo hazituvunji moyo maana tunaye Kristo ndani yetu aliyesema tumtwike fadhaa zetu zote na mzigo yetu.Mara nyingi tunapofika mwisho wa akili zetu na maarifa yetu ndipo Mungu huanza kutenda na tuka mshangaa.


  • Upinzani hauwezi Kumfanya mwenye haki atelekezwe.


Pamoja na upinzani na mateso bado wenye haki hatuachwi na kutelekezea na Mungu wetu.Neno kupingwa alilolitumia Paulo kiyunani linatafsiri ya kuwindwa,Ni kama vile mwindaji anavyo mfukuzia mnyama.Ni kama vile shujaa anayejua kuwa anafuatwa kila anakoenda,ingawa hawaoni adui zake,lakini wapo wanamfuatia kila anakoenda.

Paulo  alijua hili kutokana na uzoefu wake bianfsi.Kila mahali alipokwenda wapinzani wake wa kiyahudi walimfuata.Walimfuatia nyuma na kumshambulia tabia yake,mahubiri yake na kukejili ujumbe wake na kuchochoea na kupanga upinzani ndani na nje ya kanisa.Hawakumpa nafasi ya kupumzika.

Unapokuwa mwenye haki  na unapo panga kufanya jambo lolote jema au zuri katika ulimwengu huu, kuna mtu mmoja  yupo tayari kukupinga. Unapoaamua kujitoa kwa kusudi fulani la Kristo,unaweza kutarajia watu wa karibu na wewe kutokubaliana na uamuzi wako.
Katika vipindi vigumu vya upinzani watu wengine wanaweza kututelekeza lakini hatuwezi kutelekezwa na kuachwa na Mungu. Hatukimbiwi na kuachwa tumesimama wenyewe.Hatima yetu Wenye haki haitelekezwi.Mungu yupo pamoja nasi.

Katika upinzani tunaweza kudhani tunamalizwa lakini ni kinyume chake kabisa.Upinzani hutufungulia fursa, Paulo anakiri hili katika I Wakoritho 16:9.Kwa maneno haya, “ kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao”.Nakubaliana na Bob Jones Sr aliye wahi kusema maneno haya,  “ Milango ya fursa huyumbia kwenye bawawa za upinzani”

  • Mashambulizi makali hayawateketezi  wenye haki


Wenye haki wanaweza kushambuliwa na kupingwa lakini hawateketei kama mitende wanaendelea kusimama imara katikati ya dhoruba.Wanaweza kuangushwa chini lakini hawamalizwi.

Ukiwa mwenye haki na ukiishi muda mrefu utagundua kwamba katika maisha  kuna kushambuliwa kwa ghafla na dharura usizozitarajia, matukio ambayo hukuyaona yakija, na majanga ambayo yanaonekana kutokea kule kusikoonekana. Lakini pia matetemeko ya matatizo yatatikisa maisha yako.Kwa kifupi yale yanayowatokea wengine yanaweza kututokea na sisi pia.

Ni makosa kufikiria kwamba Mungu ametuahidi wenye haki wake Kinga dhidi ya matatizo.Daudi anasema, “Mateso ya Mwenye haki ni mengi ,lakini Bwana humwokoa nayo yote”
Mtu yeyote yule anaweza kuimba wakati jua linawaka na kung’ara, Mwenye haki  yeye huenda mbali zaidi na huweza   kuimba  hata katikati ya usiku wa manane, na Ulimwengu utamsikia yeye kwa namna tofauti.

 Meinrald Athony Mtitu
  Light of Hope Teaching Ministries- LHTM




No comments:

Post a Comment

KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI

Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea...