Mambo Ya matano ya Kufanya Unapokuwa Umebarikiwa
Na Kuwa Na Pesa Nyingi
Na Kuwa Na Pesa Nyingi
Utajiri unapaswa kuwa Baraka na sio laana,ukishindwa kufuata maonyo haya utajiri utageuka kuwa laana badala ya Baraka.Kama huwezi mambo haya achana na habari za kutaka kuwa tajiri maana utajiangamiza mwenyewe.
1.Ukiwa
Tajiri Unapaswa Ushinde Tabia Ya Kujivuna
Paulo anaandika kwa kusema moja ya jaribu la
kulishinda ukiwa tajiri ni “kujivuna”, au ”kujiona”.
1
Timotheo 6:17
Waagize
wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini
lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu
ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie.
Utajiri
unatabia ya kuzalisha kiburi,hatusemi kwamba kila tajiri ana kiburi,wapo
maskini pia na wana kiburi.Kiburi cha tajiri ni katika vile alivyo
navyo,atataka kuheshimiwa, kutambulikwa,
kutofautishwa na wengine ,n.k.
Kadiri
unavyokuwa na fedha nyingi na mali nyingi ndivyo unavyopaswa kuomba zaidi kuwa
mnyenyekevu. Kama wewe ni tajiri unahitaji wakati wote kujikumbusha kuwa
mnyenyekevu mbele za Mungu na watu wengine.
2.Usiweke Matumaini Katika Mali Zako
I TIMOTHEO 6:17 b
“wala
wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao
katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie.”
Pamoja
na mali zako usiache kumtumaini Mungu ,hili ni jaribu kubwa sana tuna pokuwa na
fedha nyingi na mali nyingi.Ndio maana tusipende tu na kufurahia kuhubiriwa
kuwa tutakuwa matajiri,tutapewa upako wa utajiri,lakini wahubiri hawatufundishi
juu ya changamoto na majaribu ya kuwa tajiri.Wanatuhubiria tutakuwa matajiri lakini hawatufundishi
tutaishi vipi tukiwa matajiri,mtindo wetu wa maisha utakuwa vipi tukiwa
matajiri.
Ni
rahisi sana kuwahubiria watu na kuwaombea wawe matajiri lakini ni vigumu sana
kuwaambia ukweli uliojificha nyuma ya kuwa matajiri.Hapa Paulo anawaambia
ukweli bila kuficha,pia anasema ukweli
juu ya changamoto za utajiri.Ni
rahisi sana kutumainia mali zinazo shikika tulizo jikusanyia. Najua fedha
zina weza kununua bidhaa na huduma mbalimbali.Fedha ina nguvu sana kiasi ya
kwamba ni rahisi sana kudanganyika kufikiria
ya kwamba itaweza kutupatia mahitaji yetu yote na kutupa ulinzi na usalama.
Fedha inaweza kuwa upendo wetu wa kwanza.katika hali ya kawaida tunavutwa
zaidi kutumainia vile vinavyo onekana kuliko Mungu asiye onekana. Ndio maana
tunapaswa kujikumbusha kuenenda kwa imani zaidi kulilo kwa kuona.
3.Uwe Mtoaji Kwa Ukarimu.
I TIMOTHEO 6: 17- 18
Waagize
watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, pia wawe wakarimu na walio
tayari kushiriki mali zao na wengine. Kwa njia hii watajiwekea hazina kama
msingi kwa ajili ya wakati ujao na hivyo watajipatia uzima, yaani, ule uzima
ambao ni wa kweli.
Kinga
kubwa yenye mafanikio ya huu ugonjwa wa kupenda fedha ni kutoa kwa ukarimu,weka kiwango ambacho unataka kujikumiliki,na baada ya
kufikia lengo lako ,toa kwa ukarimu kinacho bakia Salia kwaajili ya ufalme wa
Mungu,Hapa utakuwa salama kiroho.Moja ya jaribu kuwa ambalo tunapaswa kulikwepa
ni kadiri tunavyo pata fedha zaidi na zaidi ndivyo tunavyo jaribiwa kuzitumia
kibinafsi kwaaji yetu wenyewe.
4.Epuka
matumzi ya anasa
Mungu hana shida na
wewe kuwa na fedha na mali,ana shida na vile unavyotumia fedha yako na mali
yako.Yakobo anashambulia kwa matajiri ni vile wanavyotumia utajiri
wao,wanavyoishi kwa anasa na kufua fedha kwa matumizi ya anasa.“Mmeishi duniani kwa anasa na kwa starehe,
mmejinenepesha kama vile katika siku ya karamu.” YAKOBO 5:5 .Neno anasa (spatalao) ni
neno la kiyunani lenye kumaanisha anasa iliyopiti kiasi.
LUKA
16:19 Katika habari hii,Tajiri alikuwa
anaishi kwa anasa kila siku wakati
Maskini lazaro alikuwa anateseka nje ya geti lake. Ni makosa kufurahia anasa na kuzuia kile ambacho ni
haki ya wengine au kushindwa
kuwasaidia wengine waliokuzunguka wenye
mahitaji. Kwa upande mwingine hatupaswi kwenda kwenye kupitiliza sana na
kuwahukumu wakristo kwa kufurahia kazi ya mikono yao
5. Epuka
Kujilimbikizia Mali
Kuna
tofauti kati ya kujiwekea akiba na kujirimbikizia mali,ambako ni kunasukumwa na
ubinafsi na umimi zaidi .
YAKOBO
5:1-3
“Basi
sikilizeni, ninyi matajiri, lieni na kuomboleza kwa ajili ya hali mbaya sana
inayowajia. Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu
na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila
miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho.”
Neno
kujiwekea hazina katika lugha ya
kiyunani ni thesaurizo, Ni neno linalotupa neno la kiingereza
Thesaurus,lenye maana ya mkusanyiko wa maneno.Hapa Yakobo alikuwa anaonya walio
matajiri walio na fedha nyingi kuto jirimbikizia vitu.
Yesu anatuona dhidi ya kujilimbikizia
fedha na mali katika Luka 12:15, anasema
“Ndipo
Yesu akawaambia, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana
maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.”
Hakuna
tatizo kama tunaweka akiba kwa kusudi iliyo halali, Kuchakuri hutunza karanga
ili aweze kuwa na kitu cha kula kwa mwaka mzima,chungu,mchwa n.k.Kuweka akiba
fedha kwaajili ya matumizi
yasiyotarajiwa ni busara na akili.
Mungu hakubariki ili
uhodhi na kulimbikiza,anakubariki ili uwe chanzo cha Baraka zake wa wengine. - Carlos Wilson
Kuweka
akiba kwaajili ya usoni ni bora kulilo
kukopa fedha wakati utapokuja.Biblia
haikatazi kujiwekea akiba na kuweza,lakini ina kuhukumu vikali
kujilimbikizia.Kujirimbikizia hakupaswi kuondoa imani kwa Mungu.Watu
wanaojilimbikizia mara nyingi hujikuta wanaondoa imani yao kwa Mungu kama
mtoaji.
Yesu
alionya sana juu ya kujilimbikizia fedha
kibinafsi,.Mungu hatoi utajiri ,mali ili ilimbikizwe bali itumike na
wengine.Badala ya kujiwekea hazina Mbinguni kwa kutumia hazina zao kwa manufaa
ya wengi walikuwa kwa ubinafsi wanajilimbikizia wenyewe kwa usalama wao na raha
zao wenyewe.
Meinrald Mtitu.
No comments:
Post a Comment