KUSTAWI KAMA MTENDE.
“Mtende
huwa kijani kibichi wakati wote na wenye utomvu hii ni alama ya Neema,
ustawi,mafanikio na afya”
ZABURI 92:14b
Watajaa
utomvu, watakuwa na ubichi.
M
|
tende
ni mti wenye upekee wake. Ni mti wenye ukijani kibichi wakati wote wa Mwaka.Wakati miti mingine ya
kawaida si ya kijani kibichi wakati wote wa mwaka,Mingi hunyauka na kupukutisha
majani na wa kwa miezi tisa huonekana kama vile
imekufa ,haina ukuaji wala mafanikio lakini sio Mtende .
Mtende
ni mti wa kijani kibichi wakati wote na uliyo jaa utomvu.
Mtende
huwa kijani kibichi wakati wote na wenye utomvu hii ni alama ya Neema,
ustawi,mafanikio na afya tele.
Tafsiri
za kiingereza zimetumia neno mafuta
(fatness) zikielezea utomvu.Hivyo utomvi unawakilisha wazo la utajiri na mali na
mafanikio.Neno hili utomvu linatokana na neno la kiebrania “dashen” ambalo lilitumika kuelezea mafuta ya wanyama.Hivyo neno hili
linazungumza kukubalika mbele za Mungu kama ambavyo sadaka ya mafuta ya mnyama ilivyookuwa
inakubalika.
Neno
kustawahi limetajwa mara tatu katika mistari
hii 12-13,Maneno haya katika Kiingereza na Kiswahili ni kama neno moja lakini katika
kiebrania ni maneno tofatuti.Neno
la kwanza ni Parach lina maana ya ukuaji
wa mara moja ( Spontaneius growth), inazungumzia
juu ya kitu si kilichotokeza,lakini kilicho chanua mara moja. Hapa kuchanua mara
ndio kuliko tafsiriwa “kustawi” au “flourish”.Mstari
wa 14 neno la kiebrania linalotumika kutafsiri kustawahi (flourishing), ni tofauti lina
maana ya“ ukuaji Endelevu”.Siyo kitu fulani kina chomoza juu kwa mara moja
na kufa usiku mmoja,lakini ni kitu kinacho chomoza na kipo tele na kina endelea
na kuendelea.
KWELI YA KIROHO
kama
vile Mtende unavyostawi na kufanikiwa
kwa kuwa kijani kibichi na wenye utomvu wakati wote ndivyo vile Mwenye
haki naye anapaswa kuwa na maisha
ya kustawi na kufanikiwa.
Mungu
anataka watu wake wawe na uhai wa kiroho na ustawi katika muda wetu wa kuwepo
duniani.Anatutaka tuwe kama Mtende, tuwe wakijani kibichi,tukionyesha alama ya
uzima na tukiwa na mafanikio katika wakati wote wa kuhusiana kwetu na Mungu
mwenyenzi na maisha yetu ya kiroho ndani
ya Kristo Yesu.
Maana ya mafanikio
Mafanikio
ni neno maarufu sana leo ndani na nje ya kanisa,lakini ni moja ya neno lenye kutumiwa vibaya na kueleweka
vibaya zaidi. Mwenye haki anategemewa kuwa na mafanikio Kiroho na Kimwili
pia.Ndani ya Kristo kuna utajiri wa baraka za rohoni na mwili,ndani ya Kristo
kuna utajari wa uzima.Paulo anaeleza juu
ya utajiri uliopo ndani ya Kristo.
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri
ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Mafanikio sio kuwa na fedha tu au mali nyingi,kama ambavyo wengi
wanatafsiri. Pia utajiri ni zaidi ya kuwa na mali na vitu.Kwa mujibu wa kamusi ya
Webster na tafsiri kadhaa zinazopatika katika kiyunani na kiebrani .Neno mafanikio lina maana pana,hapa ni baadhi
ya mambo yanayobebwa na neno hili.
- Mafanikio ni pamoja na kuwa na uwingi,kuwa juu na zaidi ya, kujaa.
- Mafanikio nikwenda mbele au kuongezeka katika kila kilicho chema au kinachotamanika
- Mafanikio ni pamoja na kufunguliwa,kuwa na wokovu,kuwa na Amani.
- Mafanikio ni pamoja na kuwa na ziada na siyo kile cha kutosha tu.
- Mafanikio ni pamoja na kuendelea mbele katika biashara au shughuli fulani.
- Mafanikio ni kuwa kamili na kukamilikaMafanikio ni kuwa na bahati njema,kuwa na neema,Baraka,ustawi,mali
Mafanikio Ya Mwenye Haki
Yohana anazungumza kuhusu kufanikiwa kwa Mtu wa Mungu.Mungu anataka
sisi wenye haki tufanikiwe katika
roho,nafsi,Mwili na katika mambo yote mengineyo .
3 YOHANA 2:1-2
Mzee,
kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpenzi
naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako
ifanikiwavyo.
Yohana
alimwombea Gayo kufanikiwa katika nafsi ,kufanikiwa katika vitu na katika
afya,yaani mwili wake.Na inaoneka Gayo alikuwa tayari anafanikiwa vizuri katika
nafsi /roho yake.
Mafanikio ya kiroho kwa
mwenye haki
Kwa mujibu wa
mafundisho ya Yesu ni mafanikio ya nafsi
na roho ya mtu ni ya muhimu na ndiyo ya kupewa mkazo na kipaumbele cha
kwanza.Yesu alisema hivi, “Itamfaidia
nini mtu akiupata ulimwengu mzima kisha akaipoteza nafsi yake?”. Ni wazi alikuwa
anamaanisha mafanikio ya nafsi na roho ni ya muhimu zaidi.
Mafanikio ya roho yako
yanahusiana na mahusiano yako na Mungu. Mafanikio ya roho yana husiana na namna
gani tuna utajiri katika uzoefu wetu na Mungu.Moja ya sehemu ya mafanikio ya
kiroho ni pale tunapo ongeza maarifa yetu juu ya Mungu kama vile Mtume Petro
anavyo shauri katika
2 Petro 3:18.
“Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.”
2 Petro 3:18.
“Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.”
Kama
hatufanyiki zaidi kuwa kama Kristo,basi hatuwezi hatumpendezi Mungu.Kuwa kama
Kristo ndilo lengo letu la kikomo kwa nafsi zetu.
Mafanikio
ya roho ni kufuata maisha ya kuwa na haki ambayo inapatikana na kuhesabiwa
ndani ya Kristo tu. Kama haufanikiwa katika nafsi yako na roho,basi mafanikio
mengine yote ya vitu na mwili hayana maana sana
Mafanikio ya Mwenye haki katika Mambo Mengine yote
Kuna mafanikio kwa mahitaji yako mbalimbali kutimizwa na kukidhiwa.Ni
kimaandiko kila moja kujitahidi kuishi maisha ya kujitosheleza na kutowalemea
wengine na hata kufanya Ukristo utazamwe kwa jicho baya na wale wasio amini( 1 Wathesalonike 4:11-12),
Kwa mwenye
haki kuwa na Mafanikio katika mambo mengine yasiyohusu nafsi na roho Kuna kuja kwa kumtafuta Mungu
kwanza.
Mafanikio katika mambo yote yana
husisha kazi,biashara,mali,vitu,n.k. Ni ahadi ya
Yesu katika Mathayo 6 :30-33
kama Tukitafuta kwanza ufalme wa Mungu haya mengine ambayo tunaya hitaji kama
watu wengine wanavyohitaji tutazidishiwa. Mafanikio mengine ni
pamoja na kuwa na afya njema.kutougua na kuwa mbali na magonjwa.
Mambo
ya kufanya ili mwenye haki aweze kufanikiwa
1.
Tafuta
kwanza haki yake Mungu kwa bidii
Neno haki lina maana ya kuwa kusimama
sawa na Mungu.Kuwa na haki ni hari ya kiroho ya unyofu ambayo inaweza kufikiwa
kwa kupitia kumwamini Yesu na Mpango wa
Mungu wa Wokovu.Kuwa
Mwenye haki haina maana ya kwamba wewe ni makamilifu,lakini ina maana kwamba
unafuata Njia za Mungu na unaamini katika Wokovu. Maana yake wakati wote
unazitafuta njia za Mungu na kuziishi katika maisha yako mwenyewe.
Katika Zaburi
37:25-26 Daudi anasema hajawahi kumwona mwenye haki ameachwa au wazao
wake wakiomba chakula. Unapoenenda
katika maisha ya haki,Mungu hawezi kukuacha,utabarikiwa na kustawi. Mungu
atahakikisha anatimiza mahitaji yako ya msingi.
2. Tembea katika njia za Bwana na kuzifuata.
Maelekezo ya Daudi kwa Solomoni wakati
anakaribia kufa ilikuwa ni kama akitembea katika njia za Bwana basi atafanikiwa
katika mambo yote atakayoyafanya.Mwenye haki anapofanya mambo ya kimungu na
kufuata njia za Mungu atafanikiwa katika
kila analolifanya.
I Wafalme 2:3
3. Tembea katika haki na unyofu
Mungu ni Jua na
ngao.Kutembea katika haki katika njia ya Bwana
huruhusu Mungu kuangaza katika njia zetu kama Juan a kutukulinda kama
ngao.Hii inamfanya yeye kuongeza neema kwako pale unapohitaji na inamfanya yeye
kuleta vitu vyote vyema na vizuri katika njia yako. Zaburi 84:11-12
4. Tambua Baraka zote zinatoka kwa Bwana na hazina majuto:
Bwana ni mtoa
Baraka.Unapataje Baraka za Bwana juu yako,jibu ni kwa kufuata njia zake,kuwa na
bidii,kumtafuta yeye , na kutafuta haki yake. Baraka zake zinakutajirisha kila
eneo na anazitoa bure na kwa furaha kwako.Mithali 10:22
5 5. Tambua
nguvu ya utajiri inatoka kwa Mungu
Mungu
ana nguvu za utajiri na ndiye anayetoa au kutuoa nguvu hizo.Kumbuka utajiri
wote unatoka kwa Mungu.Yeye hutoa nguvu za kuzalisha ,kutengeneza utajiri,uwe
kidogo au mwingi.Tambua utajiri unapatikana wa Nguvu zake na sio kwa nguvu zako
na hivyo ubakie mnyeynyekevu. Kumbukumbu la Torati 8:17-18
Utambuzi huu
unamfanya Mungu akufungulie milango na kubariki kazi yako.Unapomtoa Mungu
katika mahesabu unazizuia Baraka zake katika kazi yake yote haijalishi umeweka
bidii kiasi gani,Hawezi kuzidisha isipokuwa umeanmini kwampo mwishowe vyote
hutoka kwake.
6.
Fanya yote yaliyosawa
kwa moyo wako wote na kwa uaminifu
Hezekia alimtafuta Mungu na kufanya
yaliyo mema na kumtumikia kwa moyo wake wote.Pale unapomtafuta Mungu katika
kila hali na ukadumu katika uaminifu Mungu atasababisha ufanikiwe kwa namna ile
ile.
2 Mambo ya Nyakati
31:20-21
7.
Furahia Neno la Mungu na kulitafakari wakati wote
Kushirikiana na waovu na kufuata mashauri yawasio
haki ni mambo yatakayozuia Baraka za Mungu kukujia.Lakini unapouweka moyo wako
na akili yako wakati wote ikiwa
imetunzwa na kuliwashwa,siku zote itakuwa na matunda na utafanikiwa kwasababu una
yo ile Baraka ya Mungu juu yako. Zaburi 1:1-3
Utakuwa na matunda kwa wakati wake.Hauta nyauka
pale mambo yanapokuwa magumu katika msimu wa ukamae.Utafanikiwa katika kila
ulifanyalo pale unapodumu kutafuta mambo ya Kiungu.
2 Mambo ya Nyakati 26:5
Ninasema jambo kwenu nyote pia natoa salamu zalambi lambi Mungu akubariki ndugu Pastor Meinrald Antony Mtitu kwa vitabu vyenu ambavyo vimekuwa faraja kwangu.Tunaomba kujua namna ya kuweza kuvipata hivyo vitabu.
ReplyDelete