Haitajilishi nini unapitia wewe Dumu Katika Kuabudu Na Kumsifu Mungu Kwa Moyo Wako Wote.
Sifa ni moja ya
silaha katika ghala ya silaha za Mkristo ambayo Shetani hawezi
kujilinda nayo.Tunapomsifu Mungu tunakiri kwamba Yeye ndiye anayetawala,anaweza
kufanya kile anachotaka,wakati anaotaka na kwa namna anayotaka.
Kusifu ni zaidi ya
kumkiri Mungu kwa yale mema yanayotujia.Kusifu ni kupokea kutoka kwa
Mungu yote yanayotujia,mema na mabaya.Sifa tunazotoa pale mambo
yanapoenda ndiyo siyo upande wetu zina thamani zaidi na nguvu kuliko zile sifa
tunazozitoa wakati mambo yote kwetu ni mazuri.
YEREMIA. 20:13
Mwimbieni BWANA!
mpeni BWANA sifa! Huokoa uhai wa mhitaji kutoka mikononi mwa waovu.
Katika Maandiko haya
Yeremia alikuwa katika wakati mgumu kabisa wa maisha yake lakini tunaona Kukata
tamaa kwa Yeremia kuligeuka kuwa ni furaha.Hali yake ya kushindwa iligeuka kuwa
ushindi,na kufadhaika kuwa ujasiri.Funguo inayofungua mlango wa ushindi ilikuwa
ni kusifu. Yeremiah kwa ushindi alitangaza , Mwimbie
Bwana,Bwana Asifiwe.
Haijalishi nini unapitia
sasa,endelea kumsifu Mungu.Paulo na Sila ni mfano wa watu walioendelea kumsifu
Mungu wakiwa katika mazingira magumu gerezani.Watu wengi tukiwa katika
matatizo,adha, au mateso fulani tunakuwa kama wana waisraeli walio kataa
kumwimbia Bwana katika Nchi ya Ugeni.
Zaburi
137:1-4
Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia
tulipoikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika
vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na
waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje
wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni?
Kuna nguvu kubwa
iliyojificha nyuma ya sifa hasa wakati tumevunjika moyo.Kuna mambo makuu manne
ambayo sifa huyafanya ;
1. Kusifu kuna
mtambua Mungu kama yeye ndiye Mpaji na mtoaji wako
Sifa zinafanya akili
zetu zihame kwenye hali yetu na kuzielekeza kwa Mungu.Sifa zina mpa Mungu haki
ya kutawala na kumili maisha yetu vile anavyoona Yeye inafaa.Sifa
zinakubali na kukiri kwamba Mungu anajua zaidi kuhusu kile anachofanya kuliko
vile sisi tunavyojua.Sifa zina kubali kwamba Mungu anaweza kuchukua mambo yote
yaliyo mabaya katika maisha yetu na kutoka haya akafanya kitu kizuri.
2.Kusifu kuna fanya mpango wa Mungu kwako uwekwe
wazi.
Katika Yeremia 29:11
,tunasoma hivi; Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,’’
asema BWANA. “Ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango
ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.
3.Kusifu kuna ipokea hali iliyopo sasa kama sehemu
ya mapenzi ya Mungu kwetu.
Sifa zina msingi katika
kupokea kwa kikamilifu na kwa furaha hali ya sasa kama ni sehemu ya
Upendo wa Mungu kwetu na mapenzi yake kamili kwetu.Sifa hazitegemei
nini tunafikiri au tunatumaini kitatokea huko mbeleni.Tunamsifu Mungu,sio kwa
kile tunachotarajia kitatokea kwetu,bali tunamsifu Yeye kwa Vile alivyo
na kwa pale na namna tulivyo sasa.
4. Kusifu kunaachilia nguvu za Mungu kutembea
katika maisha yetu.
Maombi yanafungua malngo
kwa nguvu za Mungu kutembea katika maisha yetu.Lakini maombi ya sifa
yanaachilia zaidi nguvu za Mungu kuliko aina yoyote ya maombi ya dua.Mungu
anakaa na anaishi na kufanya makao katika sifa za watu wake,Mtunga Zaburi
anaandika hivi,
Zaburi 22:3
Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.
Nguvu za
Mungu na uwepo wa Mungu upo karibu pale tunapo msifu
yeye.Wakati tunapo msimu Mungu kwa hali iliyopo kama ni
sehemu ya mpango wa Mungu,nguvu za Mungu huwa zinaachiliwa,Nguvu ya Mungu hii
haiwezi kuletwa kwa sisi kuwa na mtazamo mbaya au kuamuliwa na juhudi zetu
binafsi,lakini ni kwa Mungu kutenda kazi katika maisha yetu.
Mara nyingi tunapokuwa
tumekata tamaa huwa hatujisikia kumtukuza Mungu, tunahisi kama hayupo karibu
nasi na ametuacha pekee yetu. Mungu yupo haijalishi unasijikiaje.Kiwango cha
kina sana cha kuabudu ni kumsifu Mungu hata katika wakati maumivu
yako makali sana.
Mungu siku zote yupo hata pale tunapokuwa hatuna
habari naye,na uwepo wake ni wa ajabu mno hauwezi kupimwa na hisia zetu.Hivyo
Tuendelee kumshukuru Mungu hata wakati wa kukata tamaa na kuvunjwa moyo,
tuendelee kumwamini tunapojaribiwa na kujisalimisha huku tunaumia na
kuendelea kumpenda hata pale anapoonekana kuwa Yu mbali nasi.
Meinrald A. Mtitu
Light of Hope Teaching Ministries
No comments:
Post a Comment