ALAMA
ZA ROHO MTAKATIFU
Kutokana na utendaji na
madhihirisho ya kazi na huduma za Roho
Mtakatifu, imempendeza Baba kwamba Roho Mtakatifu awe na alama zinazo
mwakilisha.Alama hizi tofauti zinaweka wazi asili,tabia na kazi za Roho,kama
vile ilivyo kwa alama za Yesu Kristo ,Mwana wa Mungu.
Alama 15 Za Roho Mtakatifu.
- ALAMA YA MAJI
Alama ya hii ya maji inapotumiwa kwa Roho Mtakatifu inawakilisha
juu ya utoaji wake wa uzima unaotiririka unaoleta uahi mpya,pia inawakilisha
kazi yake ya kuosha na kusafisha na kuzaa matunda. Maji ni alama ya Roho
Mtakatifu kwa maana ya kuwa mito itatoka
ndani yetu baaad ya kubatizwa katika Roho Mtakatifu.(Yohana 7:38,39, 4:4,
Zaburi 72:6, 87:7, Isaya 44:3, Kutoka 17:6, I Kor.10:4)
2.ALAMA YA MOTO
Alama hii ya moto
inatumika kuonyesha utakatifu wa Mungu ambapo Roho Mtakatifu anahusika kuhukumu
na kusafisha na kutakasa kama moto.Roho anashuhudia , kuhakikisha na kuhukumu
dhambi. Ubatizo wa Roho huambatana na moto wa kiroho .(Mathayo 3:11, Matendo
2:3, Isaya 4:4, Kutoka 19:18, Malaki
3:2-3, Waebrania 12:29)
3.ALAMA
YA UPEPO AU PUMZI.
Alama hii inaashiria utoaji wa uzima wa pumzi ya Mungu katika nguvu yake ya kutoa
uhai mpya.Hii inasisitiza ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Nafsi isiyo onekana
lakini bado athari za utendaji wake zinaweza kuonekana. ( Matendo 2:2, Yohana
3:8;Ezekieli 37:9-10 ,Isaya 40:7)
4. ALAMA
YA UMANDE
Alama hii inaashiria kazi ya Roho
Mtakatifu ya kulifariji na
kulichangamsha kanisa. kulifanya liwe hai wakati wote.( Zaburi 133:1-3, Hosea
14:5)
5.ALAMA
YA MAFUTA
Alama hii ya Roho
Mtakatifu inazungumza juu ya mambo haya yafuatayo;kuwekwa wakfu na Uwezo wa
Kimungu wa Roho Mtakatifu,Neema ya upako,Uwepo wake wa Uponyaji, na Mwangazio
wa mafundisho yake.Ni Roho ambaye huwatia mafuta(kuwateua na Kuwasmika) waamini
wa kanisa kwaajili ya kazi za kitumishi. (Luke
4:18, Matendo 10:38, 1 Yohana
2:20,27, Zaburi 23:5
6. ALAMA
YA NJIWA.
Alama ya njiwa inatumika kuwakilisha usafi,uzuri,upole, Amani na asili
na tabia za Roho Mtakatifu kwa Ujumla.(Mathayo 3:16, Luka 3:22,Mwanzo 1:2,
Mathayo 10:16)
7.ALAMA
YA MHURI.
Mhuri ni alama ya umuhimu ya kuonyesha umiliki,na
usalama.Alama hii inasisitiza juu ya
kazi ya Roho Mtakatifu ya kututhibitisha mbele za Mungu kwamba Yeye
Anatumiliki,tu wake,na ana mamlaka juu yetu na usalama wetu upo kwake. (Efeso
1:13,4:30, 2 Kor. 1:22, 2 Timotheo 2:19)
8.ALAMA
YA SAUTI NDOGO YA UTULIVU.
Roho ni sauti
ya Mungu ndani ya mtu inayoleta ufunuo wa mapenzi ya Mungu kwake.Mwanzo 3:8, 2
Wafalme 19:11-13
9.ALAMA
YA KIDOLE CHA MUNGU.
Roho ndiye anayeonyeshea kidole cha kumshitaki
mwenye dhambi ,kumfanya avutwe na kukujisikia mwenye hatia hata kumpelekea
ampokee Yesu Kristo kama mtetezi wake(wakili wake) Luka 11:20, Mathayo 12:28
Malimbuko ilikuwa ni
alama ya mavuno kamili yanayokuja, Alama hii inaonyesha vile kazi ya awali ya
Roho Mtakatifu ya kuifanya upya roho ya mwamini(kuzaliwa mara ya pili)
inapelekea kwenye wokovu kamili na kutukuzwa kwa mwamini mbele za Mungu. Warumi
8:23
11.ALAMA YA DHAMANA
Dhamana Ni malipo ya
mwanzo yanayo ashiria malipo kamili yatakayafuatia.Alama hii ni kuonyesha vile Kazi ya Roho katika wokovu
wetu ni sehemu ya mwanzo ya kazi kamili na kuu ya ukombozi utakao kuja.Alama
hii inafanana na ile ya malimbuko. (Efeso 1:13-14, 1Kor. 1:22)
12.ALAMA YA VAZI AU KUVIKWA
Alama hii ya kuvikwa inamaanisha kumvaa Roho
Mtakatifu,yaani Roho kuwa juu ya mtu.Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kama kuvaa
vazi la kiuungu kutoka juu.Ni vazi la mwamini kwaajili ya huduma mbele za
Bwana. (Luka 24:9,Waamuzi 6:34, Isaya 61:10,)
13.ALAMA YA NAMBA SABA.
Namba saba inatumika kuhusisha ufunuo wa Roho
Mtakatifu,Ni alama ya ukamilifu,kukamilika ,na kamili,Inawakilisha ukamilifu wa
utendaji wa Roho katka ulimwengu. Taa saba,Macho saba,pembe saba,Roho saba . (Ufunuo
1:3-4,4:5,5:6)
14.ALAMA YA NURU
Roho ni Nuru.Taa saba
hizi ni alama za Mwangazio,ufunuo,na uvivio wa Roho Mtakatifu. Macho saba , Macho saba ni alama ya kuona,
ufahamu,kupambanua,Akili, Hii ni ishara wa Roho wa kujua yote, ukamilifu wa
kuona na kufahamu yote.( Ufunuo 1:3-4,4:5,5:6)Tunapozaliwa upya nuru huja ndani
ya mtu wa ndani kwasababu Roho wa Mungu huingia ( 2 Wakorintho 4:6 Zekaria 3:9,4:10)
15.ALAMA YA NGUVU AU UWEZO.
Pembe Saba ni alama ya
nguvu na ulinzi, zinawakilisha uwezo wote,Roho ana nguvu zote. (Ufunuo 5:6).
Roho Mtakatifu ni alama ya nguvu na uwezo utakao juu ndani ya mwamini. (
Matendo 1:8, Luka 34:49)
Pastor & Teacher
Meinrald Anthony Mtitu.
No comments:
Post a Comment