NGUVU
YA Kuzikabili dhoruba
KAMA TAI
“Washindi katika maisha ni wale
watu wanao zikabili changamato
wanazao kutana nazo bila kukata tamaa
na kuzigeuza ngazi yao ya kuwapandisha
juu zaidi katika kilele cha mafanikio”
Sifa moja
wapo ya tai ni kuwa uwezo mkubwa wa kukabiliana na dhoruba kali angani. Kwa mujibu wa kitabu cha Mithali,Katika vitu
vya kushangaza ni pamoja na mwendo wa tai anga.
Mithali 30:18-NIV- ‘‘Kuna vitu vitatu
vinavyonishangaza sana, naam, vinne nisivyo vielewa: Ni mwendo wa tai katika
anga,
…”
Tai haikimbii dhoruba ,bali
hufurahia dhoruba,ni wakati wa dhoruba kali kabisa ndipo tai anafikia mruko wa
juu kabisa,anakabiliana uso kwa uso na dhoruba kali ya upepo na mkondo
unamchukua juu hadi juu zaidi.
“Tai
ana nguvu ya kukabili dhoruba na upepo mkali
angani tofauti na ndege wengine”
Tai
anaruka kufikia mruko wa ft 15,000 kutoka usawa wa bahari, anaweza kwenda kwa
mwendo kasi wa kilomita 15-20 kwa saa. Tofauti na ndege wangine,tai anapenda
dhoruba anaweza kuihisi hata kabla hajaiona. Wakati ndege wengine wanakimbia na
kujificha tai anaruka kufuata dhoruba kwa kutumia mkondo wa hewa kupaa juu na
kuruka juu.
Mawingu
yakijikusanya tai wana furahia,wana tumia dhoruba kufikia mahali pa juu ambapo hawawezi
kufika.Mara wanapo upata upepo wa dhoruba hawatumii nguvu kupiga mbawa tena
bali wana tumia msukumo wa dhoruba inayowapiga kuranda randa katika mawingu hii
inawapa fursa ya kupumzisha mbawa zao.
Tabia
nyingine ya kipekee ya tai ni kufundisha makinda yake na kuyajaribu kabla ya
kuyaamini kuruka yenyewe. Hili ni zoezi gumu lenye maumivu kwa makinda ya
tai,lakini ndilo huwatayarisha kwa hatima ya maisha yao yote.Tai jike hukirusha
toka mwambani kiota alichoangulia na kuwabeba tai makinda katika mabawa .Wakiwa angani hugeuka na kuwa
mwaga chini nao hujitahidi kuruka.
Tai
dume huangalia zoezi lote akiona kuna kinda hawezi kuruka, yeye ghafla
huruka kwa kasi ya hadi Kilomita
100 kwa saa (kmph) na kuwaahi kumdaka
yule kinda kabla hajaanguka ardhini au kwenye mwamba.Zoezi hilo
huendelea kama mara 7-8 hivi,hatimaye tai wanaweza kuanza kupiga mabawa na
kuruka wenyewe kwa kasi ya ajabu, yote wanayopitia ni kwaajili ya kuwaanda na
maisha mapya ya kujitegemea ambayo watakumbana na dhoruba za kila aina za
angani.
Kuzikabili
Dhoruba za Matatizo Katika
Maisha.
Maisha
yetu ya kila siku yamejaa majaribu ,magumu,misukosuko na changamoto nyingi. Ni
wale wanajua kuzikabili dhoruba za maisha na siyo kuzikimbia ndio wanao ruka
juu sana na kufanikiwa.Maisha ya kiroho na kimwili yamejaa misukosuko mingi
ukiitumia vizuri ndiyo itakayo kuimarisha na kukufanya kupaa juu sana kama tai. Mungu
anatutaka tuwe kama tai ambao ambao tutajifunza nidhamu ya wakati wa
kujaribiwa.
Katika
dhoruba zote Mungu ameahidi kutubeba kama Tai anavyowa beba watoto wake angani.
KUTOKA
19:4;-
Ninyi
wenyewe mmeona nililofanya huko Misri, jinsi nilivyowabeba kwenye mbawa za tai
na kuwaleta kwangu.
Kanuni
Za Nane (8) Jinsi Ya Kuyakabili Matatizo
Kuna kanuni za kuzifahamu kuhusu dhoruba za matatizo
mbalimbali utakazo kabiliana nazo katika
maisha yako.
1. MATATIZO NI SHULE YA KUTUANDAA KWENDA KWENYE MAFANIKIO.
a) Mungu hutumia matatizo kutufundisha na
kutuandaa.
Kama tai
ambavyo huwafundisha makinda wake kuruka na hatimaye kuaminiwa ,Mungu naye
hutufundisha sisi watoto wake kwa
kuruhusu shida,taabu na dhiki na matatizo katika maisha yetu kwa
kitambo.Kupitia dhoruba za matatizo Mungu hutufundisha na kutuandaa kama vile
tai apitavyo hatua ya kuandaliwa kabla ya kuruka mwenyewe juu sana.Kabla ya
Mungu kutuamini na kutuachia kuruka kwenye mafanikio makubwa hutufundisha na
kutujaribu kwanza kwa njia mbalimbali.
b)
Kupita
matatizo tunakuwa washindi na kufanikiwa
Kila anayetaka
kufika juu sana ni lazima akubali mchakato huu wa kupitia katika dhoruba.Kupitia
majaribu Mungu
anatufundisha kuwa washindi na zaidi ya washindi,tukubali kufundishwa na
kutayarishwa kwaajili ya makusudi yake makuu aliyo nayo na maisha yetu.Paulo
Mtume anazungumza kuhusu jambo hili katika Warumi 8:30-32.
c)
Mungu
huwa nasi katika kujaribiwa kwetu
Kama
vile ambavyo tai dume huwepo karibu na
kufuatilia kinda la tai linaporuka na kuhakikisha hakuna madhara yatatokea
ndivyo ambavyo Mungu huwa nasi katika kujaribiwa kwetu.Unapoanza kuruka dhoruba
huitaji kuogopa kwa sababu Mungu yupo
siku zote karibu nawe.
Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana
humponya nayo yote. (Zaburi
34:19)
Mateso
na Magumu yanapokuja kwetu tukumbuke ni Mungu anatufundisha kuruka anataka
tutumie mbawa zetu .Mungu atakuja kutuokoa hata ruhusu kamwe tubamizwe
chini,tusilalamike wakati wa magumu,kwani tunajifunza kuruka
2. MATATIZO HUTUINUA JUU KWENYE
MAFANIKIO TUNAYOYATAKA
a)
Matatizo
yaleyale yanayo tukabili ndio hutumika kutuinua juu kwenye mafanikio na
makusudi makuu.
Dhoruba
ile ile inayotupiga ndio hutuinua juu zaidi katika mafanikio.Tai hawezi kuruka
juu bila dhoruba,shida taabu na upepo mkali ndivyo vinavyo mwinua juu.
Mara nyingi ni dhoruba
ile ile inayoonekana kutupiga huku na kule ikitaka kutuharibu kabisa ndiyo
inayotumika kutuinua juu sana katika
makusudi ya Mungu. Kama vile ambavyo
upepo makali huyapiga mabawa ya tai na kumwinua juu ya dhoruba ndivyo ambavyo majaribu
na magumu ya maisha hutuinua juu sana katika mafanikio.
b)
Matatizo
yanapaswa kutupa nguvu na kutuimarisha zaidi kuliko kutudhoofisha.
Tai hupokea nguvu kutoka kwenye dhoruba.Kadiri tai
anavyo paa juu zaidi,ndivyo anavyoweza kuruka juu zaidi. Unapokutana na dhoruba ya
upinzani hupaswi kuteteleka, bakia imara na thabiti kama tai.Usiruhusu dhoruba
hii kukuzia kufikia malengo yako uliyo jiwekea.Endelea na safari ya kupaa kama
tai,paa juu zaidi na zaidi.Wakati dhoruba za maisha zinatupiga zikabili uso kwa
uso kama tai afanyavyo,kaa katika dhoruba na ujifunze kuruka juu kwa hiyo.
Unapokutana
na dhoruba ya upinzani hupaswi kuteteleka, bakia imara na thabiti kama tai.
Pale
unapo hisia ya kwamba umefanya kila unachoweza kuizuia na kupingana na dhoruba
yako,wewe endele tu kupaa,tandaza mbawa zako kama tai na pokea mshindo toka kwa
dhoruba.Utapata nguvu kadiri ya upepo unavyo kuinua juu na juu zaidi,endelea
kupaa juu ya dhoruba kali inayokupiga ukiwa umedhamiria kufikia hatima
yako.Wakati unathubutu kupaa juu ya mawingu ya maisha ,watu wengine wanaweza
wasikuelewe,wanaweza kuhukumu bila sababu, bila kufikiria lakini wewe endelea
kupaa juu kama tai.
3. MATATIZO
HAYAKIMBIWI YANAKABILIWA
a) Usiyakimbie
matatizo bali uyakabili.
Kamwe
usiikimbie dhoruba,ikabili. Tai anajua jinsi ya kuikabili dhoruba.Wanyama
wengine wote hukimbia dhoruba inapokuja
lakini sio tai. Mtu mwenye
nguvu kama za tai lazima aipende dhoruba na asipingane na kukinzana nayo kama
wengine wafanyavyo.
Wakati
ndege wengine wana kimbia dhoruba inapokaribia na kuficha mabwa zao na
kukimbilia mafichoni ,Tai huikabili dhoruba uso kwa uso.Uwe kama tai fumbua
mbawa zako na jiandaee kupaa juu sana.
Mtu mwenye nguvu kama za tai lazima aipende dhoruba na asipingane
na kukinzana nayo kama wengine wafanyavyo.
Mara tunapogundua kuwa hakuna anayeweza kutoroka dhoruba za
maisha,mtu mwingine anaweza kutumia
dhoruba kuaamsha imani yake huwezi kuzia dhoruba lakini kama tai unaweza
kuitumia hiyo hiyo dhoruba kuruka juu sana.
b)
Watu dhaifu hukimbia matatizo
watu hali watu wenye nguvu huyastahimili.
Dhoruba inapopiga tunaweza kukunjua mbawa zetu na
kukimbia kujificha au tunaweza kumuiga
tai na kupaa juu ya dhoruba. Lazima tuwe na nguvu na ujasiri wa lazima
kukabili tufani za maisha. Tunapo kimbia kutoka kwenye dhoruba za maisha na
kutia juhudi kuzitoroka ;tuna kuwa na mtazamo wa kikawaida kama wa ndege
wengine.
Huwezi kuzuia mafuriko lakini unaweza
kujifunza kutengeneza mtumbwi na
kuogelea nao katika mafuriko.
Lakini tunapozikabili dhoruba tunakuwa na mtazamo wa kitai,basi
tunapaa na kuruka kama tai. Watu dhaifu wasio na nguvu wana tabia ya
kukimbia changamoto wanazokutana nazo katika maisha. Ukitaka kuingia katika
vitabu vya historia ya watu walioshindwa ni rahisi tu,kimbia dhoruba za maisha.
c) Ni
vigumu kufanikiwa katika maisha kama utayakimbia matatizo.
Katika
safari ya maisha huwezi kufanikiwa kama unakimbia majaribu na ugumu unakutana
nao.Watu dhaifu hulia na kupiga kelele na kulalamika na kulaumu juu ya ugumu
wakati watu wenye nguvu za tai husonga
mbele. Watu wenye mtazamo na nguvu za tai
,hugeuza majaribu kwa faida yao,huona faida katikati ya majaribu. Wakati upepo wa nguvu una piga maisha
yetu,hatupaswi kuukimbia,tusije anguka katika mianya ya maisha.
Watu dhaifu hulia na kupiga kelele na
kulalamika na kulaumu juu ya ugumu wakati watu wenye nguvu za tai husonga mbele.
Kama tai ni
lazima tujifunze kuzikabili dhoruba zetu.Lazima tupae na upepo makali
unaotupiga katika maisha kwa mbawa za maombi na imani.Hii itatupa ujasiri wa
kuzikabili dhoruba. Kaa katika dhoruba na jifunze kuruka nayo kama
Tai,maana ni dhoruba hiyo hiyo inayoonekana kukupigika na kukuteketeza ndiyo
itakayo kuinua juu sana katika Makusudi ya Mungu.
4. MATATIZO NI SEHEMU YA MAISHA HAYA
KWEPEKI
a)
Matatizo
ndiyo huyapa maisha maana.
Mara
nyingi baada ya dhoruba fulani iliyotukumba kupita, huwa hatubaki katika
viwango vilevile tulivyo kuwa navyo. Dhoruba ,yaani majaribu hutuongezea uzoefu
wetu wa maisha,dhoruba hutuongezea ukomavu wetu. Wakati dhoruba za maisha
zinavuma zikabili uso kwa uso.!
b)
Matatizo huja bila kutarajia.
Hakuna anayeyatarajia matatizo.Mara nyingi dhoruba
huja bila sisi kuzitarajia na hivyo hutukuta hatujajiandaa,dhoruba huja kwa
kasi kwa fujo na kuondoka ghafla. Ndivyo ilivyo dhoruba zinapovuma katika
maisha yetu huwa hatuzitarajii.
c)
Hakuna mtu mwenye kinga ya matatizo.
Dhoruba za maisha zinaweza kumpiga mtu
yeyote,wakati wowote na wakati wowote bila taarifa ya awali ya tahadhari. Dhoruba
za maisha hazikwepeke kila mtu atapitia
katika dhoruba fulani wakati fulani.
Kuna wakati mawingi meusi yatatanda na upepo mkali utayapiga maisha yetu,
lakini ni lazima tubakie katika kusudi letu na kupaa juu ya dhoruba. Hakuna pa
kukimbilia kutoka kwenye dhoruba za maisha bali ni lazima tusikubali kuruhusu upepo mkali kutuzuia kuziona siku zuri zijazo za jua.
d)
Shetani na watu wanaweza kutumika kutuletea
matatizo.
Tunapaswa kupigana na adui siyo dhoruba,
dhoruba siyo adui yetu,usisumbuke kutafuta dhoruba imetokea wapi. Mungu
ameiruhusu na anaweza kumtumia yeyote yule kuleta dhoruba katika maisha
yetu.Shetani ,mazingira na wanadamu wanaweza kutumika. Dhoruba huja kwa njia nyingi, kwa wengine kupitia
ugonjwa, au maafa, kushindwa, kifo, kukatishwa tamaa na maisha ,kufeli
n.k.dhoruba za maisha ni halisi!
5. MATATIZO HUWA NI YA KITAMBO NA SIO YA KUDUMU
a)
Matatizo
yote hudumu kwa kitambo fulani.
Kila
majanga ni ya kitambo tu,kila dhoruba na tufani hatimaye hupita,kila usiku
hatimaye hugeuka kuwa Asubuhi mpya. Chagua
kuvumilia na kung’ang’ania hapo mpaka uone mapambazuko ya Asubuhi yako!
b)
Usipoteze
Ndoto zako kwaajili ya matatizo ya kitambo
Haijalishi dhoruba ni kali
kiasi gani, baki umekaza kuziangalia ndoto zako na shauku zao.Ziache ndoto zako
zibaki hai, Nimapema mno kuizika ndoto yako,bado inaweza kuishi!
c)
Usipoteza
fokasi na malengo yako kwaajili ya
matatizo ya kitambo.
Thubutu
kudhamiri hatima yako na kufungua uwezo wako mkuu uliofichika. Thubutu
kutabasamu mbele ya magumu, baki na fokasi katika malengo yako, uwe tayari kwa
dhoruba kama tai.
d)
Kataa
kujihesabu umeshindwa kwasababu ya matatizo unayopitia.
Kama tai, bakia thabiti usiyeondoshwa. Kataa
kushindwa, Paa juu ya mawingu ya maisha,thubutu kuinuka juu ya dhoruba yako.Dhoruba
zote hatimaye hukoma,achilia kushindwa mkononi mwako kama vile umeshika makaa
ya moto! Amua thamani yako binafsi weka malengo na yageuze kuwa uhalisia.
e)
Katika
kila matatizo kuna mlango wa kutokea.
Katika
kila Jaribu Bwana hufanya mlango wa Kutokea .Msikie vile Paulo Mtume anavyosema ,“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya
wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo;
lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze
kustahimili.” (I
Wakoritho 13:10).
hata kama unakabiliana na dhoruba kali katika kazi
yako, ndoa au familia yako hebu usikimbie bali chukua mtazamo na fikra za tai.
Pst.Meinrald A.Mtitu.
Pst.Meinrald A.Mtitu.
No comments:
Post a Comment