SHERIA ZA KUPANDA NA KUVUNA-2
4.Sheria za kupanda na kuvuna zinatenda kazi katika pande zote mbili za mema na mabaya.
Wengi wetu tukisikia juu ya kuvuna tulichopanda, huwa tunafikiria zaidi ni kwa upande ule mbaya.Tunafikiri juu ya kulipia matokea ya matendo yetu ya dhambi au maamuzi ya kijinga tuliyofanya,lakini Sheria ya kuvuna sio tu kwa upande wa ubaya.Sheria hizi ni zipo pia kwa upande wa uzuri .Si upande wa hasi tu bali na upande wa chanya.
Sheria hizi zinafanya kazi kwa yote, mema na mabaya tunayopanda katika maisha yetu tuta yavuna.
Sheria za kuvuna zipo chanya sana,na zina simama kama ahadi ya braka kwa kupanda yale yaliyo mazuri na wakati huo huo zinasimama na kuonya kwa yale mabaya yanayopandwa.
Mungu ameweka kanuni hizi katika maandiko ili zitumike kama maonyo na kama kutia moyo.Katika Wagalatia 6:7 ,Neno lake linasema “ Msidanganyike,kila mtu atavuna kile alichopanda"
Kila mkulima anelewa maana kanuni hii;Tunavuna zaidi kile tunachopanda, na muda wa baadaye zaidi ya ule tuliopanda.
Kwasababu ya watu kuishi maisha ya uzembe na kutojalia na anasa ni kwa sababu wamedanganyika.Hawaamini ukweli,au wanafikiri Sheria za Mungu kwao zitakuwa tofauti. Sheria ya Mungu haina upendeleo inafanya kazi kwa watu wote.
Ahadi na maonyo ya Maandiko ni kwamba tunavuna kile tulicho panda.Hii ina maanisha kwamba uchaguzi katika maisha umejaa matoke yake yote mazuri au mabaya,ya muda mrefu na milele.Kuvuna kile tulichopanda kuna maanisha tunavuna tu kile kilichopanda,na tena tunavuna kwa aina ile tu tuliyoipanda,na tunavuna katika misimu tofauti na ule tulioupanda,tunavuna zaidi ya vile tulivyo panda,lakini pia tunavuna kwa kadiri tulivyo panda.
Mambo yanayotutokea sisi sasa,ni mavuno ya mawazo na matendo tuliyo panda zamani.Mawazo na matendo ya leo ni mbegu zinatazopandwa kwaajili ya mavuna ya siku zetu zijazo.
Kupanda na kuvuna ni analojia ,sahihi kabisa ya maisha yetu. NI mfano wa kitu kinachowakilisha maisha yetu.Tutafanya vema kama tutayaona maisha kama ni mchakato wa kupanda mbegu na kuvuna mavuno na kukuwa makini na kile tunacho panda.Kwa kuwa sisi sote sasa tunavuna kile tulicho wahi kupanda wakati fulani na tunapanda kile ambacho tutakuja kuvuna huko mbele,ni vizuri na muhimu sana kama tutajifunza na kuzijua kanuni hizi za kupanda na kuvuna.
5.Kuvuna na kupanda ni sheria ya ulimwengu wa kiroho
Kupanda na kuvuna pia ni sheria ya ulimwengu waroho.Ni zaidi tu ya kanuni ya kilimo.ni uhakika usio hitaji uthibitisho wa maisha kwamba tunavuna kile tulichopanda.Tunawajibika kupanda na Mungu anawajibika kwa Mavuno.Sisi tuwatenda kazi pamoja na Mungu.
Mungu hazalishi kufeli,Yeye ni Bwana wa Mavuno. Kwa sheria hizi ambazo Mungu ameziamuri,tunahitaji kupanda mbegu ambazo zitaleta matunda sasa na milele.Yeye ni Bwana wa Mavuno. Kila tunapoingia katika msimu mpya lazima tuanze na kupanda.
Kupanda na kuvuna Ni zaidi tu ya kanuni ya kilimo ,ni sheria pia ya ulimwengu waroho.
Katika Luka 6:38,Yesu anatuhakikishia kwamba tunaweza kuitumainia sheria hii.Sheria ya kupanda na kuvuna mara zote inafanya kazi,na inafanya kazi kwa namana ile ile kwa kila mtu.Kama utapanda mambo mabaya,utavuna mambo mabaya.
Katika mstari wa 37 anaanza kwa onyo la “usihukumu”.Jaribu kudhania nini kitatokea utafanya hivyo,jibu ni wazi utavuna hukumu.Kama utajiepusha na kuhukumu wengine,utajiepusha na kuvuna hukumu kutoka kwa wengine. Anasema “Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. “
Kisha katika mstari wa 38 anaendelea kwa kuonyesha utekelezaji wa sheria wa kupanda na kuvuna katika utoaji wetu kwa vitu mbalimbali; hivyo ndiyo anavyosema , “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Hii inaizungumiza hofu ya kila mwanadamu,ambayo ,ni kwamba kama nitatoa,sitabakia na kitu kwaajili yangu mwenyewe.Yesu anasema kwamba kinyume chake ndio kweli.
Toa kile ambacho wewe ndicho unakihitaji sana,na utapata zaidi. Sio tu utakuwa na vya kutosha kwaajili yako,bali kadiri unavyotoa zaidi,ndivyo utavyopewa zaidi. Kadiri upandaji unavyokuwa mkubwa,Uvunaji nao huwa mkubwa.
Kila matendo mazuri,kila tendo la huduma ambalo si la kibinafsi,kila maneno mazuri ya wema,kila nia njema,kila tabasamu la upendo,kila maamuzi ya kusamehe na kusahau, kila maamuzi ya kuwavumilia wengine yatarudia sisi, katika kipimo kizuri, kilicho shindiliwa,kutikiswa na kumwagika.
6. Kupanda na kuvuna ni sheria ya msingi katika ufalme wa Mungu
Ufalme wote wa Mungu unatendakazi katika kanuni ya kupanda na kuvuna.Kama unataka kushiriki na kuhusika katika ufalme,ni lazima upande mbegu.Kama unataka kupokea vitu vizuri ambavyo Mungu ameviandaa kwaajili yako,lazima upande mbegu maalumu kwaajili ya mavuno maalumu.
Ukristo umeanza na Mbegu iliyopana-Jina lake lilikuwa ni Yesu Kristo.Mungu alimpanda Mwanawe wa pekee na leo hii tumeongezeka na kuzijidisha na kuwa mamilioni mwa waamini wake ambao tunaitwa Wana na mabinti wa Mungu.Mungu alipanda Mbegu ( Mwana wake), na watu wote ambao wameyatoa maisha yao kwa Yesu Kristo ni Mavuno yake.
Marko 4:26–29
Ufalme wote wa Mbinguni unatenda kazi kwenye kanuni ya kupanda na kuvuna.Kama unataka kujihusisha nao na kushiriki katika Ufalme wa Mungu,nilizama upande Mbegu.Ukitaka kupokea mambo mazuri ambayo Mungu ameyaandaa kwako,lazima upande Mbegu maalumu kwaajili ya mavuno maalumu.
Sisi Tunawajibika kupanda na Mungu anawajibika kwa mavuno.Tuwatendakazi pamoja na Mungu.Mungu hazalishi kufeli;Yeye ni Bwana wa mavuno.Kwa sheria hizi ambazo Mungu ameziweka katika utaraibu wake,tunahitaji kupanda mbegu ambazo zitakwenda kuleta matunda kote sasa na kwa milele.Yeye ni Bwana wa mavuno.Tunapo ingia kila msimu mpya,ni lazima tuanze kupanda.
Kuzijua kanuni za kupanda na kuvuna itakufanya kuwa makini na maisha yako ukijua kwamba kila siku unapanda mbegu kwa maneno yake,matendo yako na mawazo yako. Kanuni hizi za kupanda na kuvuna ni moja ya ufunguo wa kuona umuhimu wa mabadiliko katika maisha yetu.
Meinrald Mtitu.
Meinrald Mtitu.
No comments:
Post a Comment