Sunday, September 24, 2017

KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI



Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu

Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtoleaje ?Kila mmoja anaweza kujifunza kutoa,lakini pia inahitaji nidhamu kuwa mtoaji.Hapa ni kanuni 21 za vile tunaweza kumtolea Mungu na hivi ndivyo utoaji wetu unavyopaswa kuwa.



1. TOA KWA UPENDO:

Upendo unapasa kuwa ndiyo kisababisho kikuu nyuma ya kutoa kwetu. Upendo unapaswa kuwa ndio Nia nyuma ya kutoa kwetu.Sio lazima tuoe kwasababu fulani,upendo hautafuti sababu ya kufaidika katika kutoa huko.Tunapotoa kwa upendo si lazima tutoe ili sisi kufaidika. Ukitaka kutoa basi toa bila uchoyo.

“ Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia” Waebrania 6:10


2. TOA KWA KUABUDU ;

Kuabudu ni tendo lolote lile linalo mpa Mungu utukufu, (I Wakoritho 10:31).Kutoa ni sehemu ya Ibada. Askofu David Oyedepo anashauri hivi ,“Toa kama sehemu yako ya Ibada kwa Mungu. Tunatoa kama kuabudu hivyo hatutoi ili kupokea,lakini uaminifu wake Mungu huturudishia Baraka kwetu.”

Hatutoi kama kucheza kamali,Sadaka sio toa na kupokea. “cash and carry”.Ikiwa unatoa tu kwaajili ya kupokea utaaishi kuvunjika moyo na hutaziona Baraka.Toa kama sehemu ya kuabudu.

Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote.” Zaburi 96:8-9

3. TOA MARA KWA MARA

Kutoa iwe ni sehemu ya maisha yako,hivyo toa mara kwa mara,kila wiki,kila mwezi n.k.Kutoa ni tabia unayoweza kujifunza ni matokeo ya kitendo unachokifanya mara kwa mara.Kadiri tunavyopata nafasi au fursa tuzitumie kuwatendea mema watu wengine.Tafuta fursa za kutoa.Ukizitafuta zitaanza kujitokeza.

“Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.”-Wagalatia 6:9-10

4. TOA KWA KUMHESHIMU MUNGU:

Kutoa ni ni njia moja wapo ya kumheshimu Mungu.Ni kuonyesha heshima mbele zako,unatambua yeye ni nani na nini anafanya katika maisha yako. “Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.” Mithali 3:9-10,

5. TOA KWA KUKUSUDIA

Toa vile unavyokusudia moyoni mwako au vile unavyoguswa na Kusukumwa.Usitoe kiholela bila kusudi.Huwezi kutoa kwa kila jambo tu,tafuta kusudi la kutoa kwako. Unataka kutoa kwaajili ya kusudi gani?,jambo gani,?eneo gani?,kwaajili ya nini? Tunatoa kwa uangalifu na kwa kupanga katika maombi.Panga kabla kusudi kabla ya kutoa.Panda mbegu yako katika udongo mzuri,usitupe tu mbegu zako hovyo.

“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” 2Wakorintho 9:7


6. TOA KWA MOYO WA FURAHA

Kutoa kunapaswa kuwa ni tendo la furaha.Usitoe kwa moyo wa huzuni bali kwa kufuraha.Hisia zako katika kutoa ziwe chanya.Kutoa hakupaswi kuwa na hisia ya maumivu au majuto kwa baada ya kutoa. “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” 2 Wakoritho.9:7


7. TOA KWA UKARIMU

Ukarimu ni kwa kujali wengine. Ukarimu ni hali ya kujali mahitaji ya watu wengine.Mtu mkarimu anatoa kwa mguso wa ndani,(2 Wakorintho.9:6,13;).Unapotoa kwa ukarimu ni kama unatawanywa,lakini ndivyo unavyoongezewa.” . MTIHALI 11 :24-25
TOA KWA NEEMA YAKE MUNGU.

Utoaji unapaswa kuwa ni matokeo ya kazi ya neema yake Mungu katika maisha yetu,kunaanza kwanza kujitoa kwa maisha yetu yote kwake ,na utoaji ni kama kujazilizia kujitoa kwetu. (2 Kor. 8:1-2,6-7, 9:9-11

2. TOA KWA IMANI

Toa kwa imani ukijua Yeye ameahidi kutupa mahitaji yetu yote,hatutapungukiwa kwa kutoa kwetu,hatutakuwa wahitaji kwasababu tumetoa ( 2 Wakor. 9:7. Wafili 4:19) WAEBRANIA 11:6

3. TOA KI- KIBINAFSI.

Unapotoa toa kama wewe binafsi.Linapokuja suala na utoaji Sio lazima tusuburi utoaji wa pamoja wa kundi au watu wengine.Kutoa kwenye tija katika ufalme wa Mungu ni kule ambako kunasukumwa toka ndani ya kibinafsi.Sio lazima tusubiri mtangazo ndipo tutoe.

( I Wakoritho 16:2)

4. TOA KWA MFUMO

Katika utoaji unayo nafasi ya kujiwekea mfumo wako ambao utautumia katika kumtolea Mungu.Hivyo toa kwa mfumo uliochagua na kujiwekea.Unaweza kuwa na mfumo wa kutenga na weka akiba ya kiasi ambacho unataka kutoa kwaajili ya Bwana ili kisitumike kwaajili ya kusudi jingine.( I Kor 16:2)

5. TOA KWA KADIRI NA UWIANO:

Toa kwa kadiri na uwiano wa ulivyofanikishwa.Katika Agano Jipya tunatoa zaidi kwa kufuata kanuni ya Neema na hiari,kwa kukusudia na kwa kadiri ya vile ulivyofanikishwa.Kadiri unavyokuwa na vingi zaidi toa zaidi.

2 KOR.8:14 Kumbu 16:17, Matendo 11:28-30 I Kor. 16:2,2 Kor:8:3,12, Marko 12:41-44,


6. TOA KUTOKA KATIKA UWINGI.

Toa toka katika uwingi wa vile ulivyo navyo..Kadiri unavyo kuwa na vingi ndivyo unavyotarajiwa kutoa zaidi.

Kumb 28:47,2 Wakor. 9:7


7. TOA KWA HIARI:

Toa kwa hiari yako na kutaka kwako mwenyewe.Maamuzi ya kutoa yaye ni ya kwako mwenyewe,toa kwa kupenda toka ndani.Toa kwa utashi wako mwenyewe ukijua unachofanya,maamuzi ya kutoa yatoke ndani yako.Usitoe kwa msisimko,kwa kufauta mkumbo au kuiga. Toa kwa hiari.( I Nyakati 29:6 Kutoka 25 :2 2 Kor.9:7)

8. TOA KWA UHURU

Toa kwa uhuru bila ya kushinikizwa kutoka nje, Usitoe kwa kufanyiwa hila,kulazimishwa,kutishiwa.

Mtihali 11:24 Warumi 11:35

9. TOA KWA UNYENYEKEVU:

Kutoa kunaanza ni hali nzuri ya ndani yako.Toa kwa unyenyekevu si kwa majivuno,kiburi au kujionyesha.Kabla ya Mungu hajaangalia sadaka yako anakuangalia wewe. MIKA 6:8 MATH.6:2-4


10. TOA KWA NIA NJEMA.

Toa kwa nia njema na na sio kwa hila ,sio kwa sababu au agenda ya siri .Nia yako ya kutoa lazima iwe ni ukarimu,upendo,kumwabudu Mungu n.k.Kutoa kwa nia ya kupokea ni kama kucheza kamali.Mungu hachezi kamali.Ezekiel 33:31, Mathayo 6:33


11. TOA KWA KUWAJIBIKA

Toa kama wajibu wako kama Mkristo.Unapotoa unatimiza wajibu wako wa kiroho. Nehemia 10:34-39 Luka 16:1,2,10

12. TOA KWA KUJIKANA

Toa kwa kujikana nafsi, unabakiwa na kiasi gani baada ya kutoa ndiko kunaonyesha ulijikana kwa umbali gani. Kujitoa kwa kujikana,Daudi alikuwa na Mtazamo huu katika kutoa kwake)hatupaswi kumtolea Mungu wetu mabaki,au makombo,tumtolee kilicho bora na kizuri.Angalia karipio la Nabii Malaki.Mtume paulo anatutaka Kila mmoja wetu anahitaji atathimini upya utoaji wake.( 2 Wakoritho 2:8 Marko 12:41-44, Malaki 1:12-14 2 Samuel 24:24)

13. TOA KWA SIRI

Pale inavyowezekana toa kwa siri.Sio mara zote lazima watu wajue ulivyotoa.Unaweza toa kwa siri na Mungu akakubariki. kutoa kuwe ni kwa usiri pale inapowezekana.Kutoa si mashindano ,kila mtu anatoa kwa kadiri ya neema na alivyojaliwa.( Mithali 21:14, Mathayo 6:2-4)

14. TOA KWA KWA SHUKURANI :

Utoaji ni sehemu yako ya ibada ya shukurani kwa Mungu.Toa kama sehumu ya shukurani kwa Mungu kwa mambo mengi mno aliyekutendea.(I Nyakati 29:9, 2 Wakoritho 9:11)

15. TOA KWA UHURU

Toa kwa uhuru bila ya kushinikizwa kutoka nje, Usitoe kwa kufanyiwa hila,kulazimishwa,kutishiwa.

Mtihali 11:24 Warumi 11:35

16. TOA KWA UNYENYEKEVU:

Kutoa kunaanza ni hali nzuri ya ndani yako.Toa kwa unyenyekevu si kwa majivuno,kiburi au kujionyesha.Kabla ya Mungu hajaangalia sadaka yako anakuangalia wewe. MIKA 6:8 MATH.6:2-4

17. TOA KWA NIA NJEMA.

Toa kwa nia njema na na sio kwa hila ,sio kwa sababu au agenda ya siri .Nia yako ya kutoa lazima iwe ni ukarimu,upendo,kumwabudu Mungu n.k.Kutoa kwa nia ya kupokea ni kama kucheza kamali.Mungu hachezi kamali.Ezekiel 33:31, Mathayo 6:33

18. TOA KWA KUWAJIBIKA

Toa kama wajibu wako kama Mkristo.Unapotoa unatimiza wajibu wako wa kiroho. Nehemia 10:34-39 Luka 16:1,2,10

19. TOA KWA KUJIKANA

Toa kwa kujikana nafsi, unabakiwa na kiasi gani baada ya kutoa ndiko kunaonyesha ulijikana kwa umbali gani. Kujitoa kwa kujikana,Daudi alikuwa na Mtazamo huu katika kutoa kwake)hatupaswi kumtolea Mungu wetu mabaki,au makombo,tumtolee kilicho bora na kizuri.Angalia karipio la Nabii Malaki.Mtume paulo anatutaka Kila mmoja wetu anahitaji atathimini upya utoaji wake.( 2 Wakoritho 2:8 Marko 12:41-44, Malaki 1:12-14 2 Samuel 24:24)

20. TOA KWA SIRI

Pale inavyowezekana toa kwa siri.Sio mara zote lazima watu wajue ulivyotoa.Unaweza toa kwa siri na Mungu akakubariki. kutoa kuwe ni kwa usiri pale inapowezekana.Kutoa si mashindano ,kila mtu anatoa kwa kadiri ya neema na alivyojaliwa.( Mithali 21:14, Mathayo 6:2-4)

21. TOA KWA KWA SHUKURANI :

Utoaji ni sehemu yako ya ibada ya shukurani kwa Mungu.Toa kama sehumu ya shukurani kwa Mungu kwa mambo mengi mno aliyekutendea.(I Nyakati 29:9, 2 Wakoritho 9:11)

Mwalimu Meinrald Mtitu

Light of Hope Teaching Ministries.


Friday, September 15, 2017

TABIA KUMI ZA MTU MVIVU




TABIA KUMI (10)  ZA MTU MVIVU

1. HUPENDA SANA USINGIZI NA KULALA KWA MUDA MREFU.

MITHALI 19:15- Uvivu huleta usingizi mzito, naye mtu mzembe huona njaa.

Kulala ni jambo la kawaida na la muhimu kwa kila mwanadamu. Kwaajili ya afya njema ya mwili na akili tunahitaji wastani wa masaa 6-8 ya kulala.Hakuna tatizo katika kulala ,tatizo ni pale kulala kunapo tumika kama kichaka cha kujifichia na kukwepa kufanya kazi.

MITHALI 26:14 Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.

Mtu mvivu huona vigumu sana kukiacha kitanda chake. Anapenda sana kulala kupita mahitaji ya kawaida ya mwili wake. Watu wenye uvivu uliojificha ndani yao wakiugua kidogo au kujisikia vibaya kidogo basi kitanda kita wakoma siku hiyo ,hawatatoka kitandani.

MTIHALI 6:9-10 Ewe mvivu, utalala hata lini? utaamka lini kutoka katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono upate usingizi!

Kuna uvivu uliojificha nyuma ya kupenda kulala sana kupita mahitaji ya kawaida ya mwili na akili.

MITHALI 20 :13

Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.


Wako watu wavivu wanaokesha usiku wanaangalia luninga kiasi kwamba asubuhi hawezi kuamka,mchana kutwa wanashinda wamelala. Hii ni tabia ya uvivu. Wako watu wavivu ambao wanapenda mno usingizi kiasi kwamba hata wakijitahidi kutega kengele ya saa (Alarm) iwaamshe bado hawawezi kuamka. Wako watu wanaochelewa mara kwa mara kazini, shuleni au kuwahi usafiri kwaajili ya safari n.k.sababu kubwa ni uvivu uliojificha katika kupenda usingizi.


2. HUWA MLEGEVU KATIKA KAZI NA KUUPOTEZA MUDA KWA MAMBO YASIYO NA TIJA.


MITHALI 18:9

Mtu aliye mlegevu katika kazi yake ni ndugu na yule anayeharibu...


Tabia nyingine ya mtu mvivu ni kupoteza muda,hajali muda kabisa. Katika zama hizi za teknolojia moja ya vitu vinavyo poteza muda ni pamoja matumizi ya mitandao ya kijamii kupitia simu za kisasa za “ Smart phone”, Michezo ya kwenye simu na komputya, vipindi vya televisheni hasa vile vya maigizo na filamu.Eneo jingine ni lile la kuwasiliana kwa simu maarufu kama ku-chat.

Kwa kuwa watu wengi walio wavivu hawana nidhamu binafsi ni rahisi sana kutekwa na kutumia muda wao mwingi sana katika maeneo hayo tena hata wakiwa kazini.

Kutumia masaa mengi kawa mambo yasiyo na tija sio tatizo kwa mtu aliye na uvivu uliojificha,haoni ni tatizo lolote kuwa katika makundi ya mitandao ya kijamii na kutumia muda wake wote huko.Hata kama ni makundi ya kujadili Biblia na mambo mengine ya manufaa, haingii akili kuona mtu yupo online na akijadiliana na kubisha kuhusu Biblia kwa masaa sita! Hivi huna mambo mengine ya kufanya?

MITHALI 14:23 Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.
Mtu mvivu utamwona yupo kwenye makundi karibia kumi ya facebook na whatsApp ,bado yupo kwenye mitandao ya Instragram,Telegram, Jamii Forum na mingineyo, na kila kundi kuna mada fulani inaendelea na anataka ashiriki kuchangia.Atafanya kazi saa ngapi?atafikiri saa ngapi?

Wavivu wengine wapo ofisini utaona wakati wote wapo kwenye mitandao,unafanya kazi saa ngapi? Huo ni ulegevu na uvivu! Kuna vitu vya muhimu zaidi katika maisha zaidi ya kuwa muda wote kwenye facebook ,Instragram na Twitter.

Kuna watu ukiwaachia kazi ya kufanya hawezi kuifanya kazi na kuikamilisha kwa wakati kwasababu muda wao wote wanaupoteza kuzungumza,kupiga stori,na mazungumzo yenyewe ni yale ya upuuzi tu.Wengine ni kupoteza muda wote kwenye simu,watapigia watu simu hata kama hawa jambo lolote la maana kwasababu tu amejiunga na kifurushi cha bei nafuu na ana muda hewani wa kutosha.Huu nao ni uvivu.



3. HUACHA MAMBO YANA HARIBIKA BILA KUCHUKUA HATUA.

MITHALI 24:30-31

Nilipita karibu na shamba la mtu mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.




Mtu mvivu hawawezi kutengeneza vitu vinavyo haribika .Watu wavivu wanatabia ya kuacha mambo yanaharibika bila ya kuchukua hatua hata kama jambo husika lipo katika uwezo wao kulirekebisha.Wana acha hata nyumba zao zina haribika na kuvuja bila kufanya marekebisho kwa wakati.Mambo madogo ambayo wangeweza kuyashughulikia yataachwa hivyo kwa muda mrefu.

Nguo inaweza kubaki imechanika au kutatuka mahali bila ya kushonwa kwa muda mrefu tu kitu ambacho ni kidogo sana.Wengine kurudishia kishikizo tu kwenye shati inaweza kuchukua miezi na anaendelea kulivaa!Wengine ni viatu vilivyotatuka vitaendelea kuvaliwa bila marekebisho.

MHUBIRI 10:18

Kama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama, kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.


Kushindwa kufanya marekebisho na matengenezo madogo madogo tu ni dalili ya uvivu uliojificha. Hii inaendana na tabia nyingine ya kuahirisha mambo tutayoiangalia hapo mbele.



4. HUJAA UDHURU WA KUAHIRISHA MAMBO BILA SABABU ZA MUHIMU.

MITHALI 22:13

Mvivu husema, ‘‘Kuna simba nje!’’ au, ‘‘Nitauawa huko njiani.


Watu wavivu hutafuta sababu za kipuuzi za kutoka kufanya kazi. Wamejaa udhuru na “visababu” vya kuwepa kufanya kazi.Nyuma ya sababu zao kuna uvivu “ uliojificha”.Wakati wote wanatafuta udhuru wa kipuuzi wa kutofanya kazi na hawaukosi!


MITHALI 26:13

Mvivu husema, ‘‘Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!”



Ukimpa kazi mtu mvivu hatakosa sababu ya kutoikamilisha. Kwa kila sababu unayompa ya kufanya kazi,yeye atakupa sababu mbili ya kwanini asifanye kazi hiyo. Mtu mvivu si wakuachiwa kufanya jambo,mwachie mtu mvivu na hakuna kitu kitafanyika.

Kauri mbiu ya watu wavivu ni “kamwe usifanye leo lile unaloweza kuliacha mpaka kesho”. Watu wavivu ni wepesi kughahiri jambo na kuahirisha jambo tena bila sababu.

Mtu mvivu huwa haheshimu na kufuata ratiba aliojiwekea mwenyewe. Kuna ushauri wa hekima unasema “Usiache lifanyike kesho lile unaloweza kulifanya leo”.Ingawa ,watu wavivu wao wanasema“Kwanini ufanye leo lile unalo weza kufanya kesho?”


MITHALI 20:4

Mvivu halimi kwa majira, kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati cho chote.


Mtu mvivu anaweza kujitetea kuna joto sana au kuna baridi sana , ingawa wengine wote wanafanya kazi katika hali hiyo hiyo ya hewa.Anaweza akaacha kufanya kazi kwa hofu ya kuumia,ingawa uwezekano wa kuumia ni mdogo sana au haupo kabisa.

MITHALI 26:16

Mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wajibuo kwa busara.


Katika Mathayo 25.kuna mfano wa Talanta,Bwana aliyesafiri kwenda nchi ya mbali aliwapa watumishi wake talanta (fedha za wakati huo) ili wazizalishe mpaka atakapo rudi.Wawili walifanya fanya bidii na kuzalisha,lakini mmoja hakufanya kitu alifukia talanta aliyopewa.Na Bwana wake aliporudi alitoa sababu za kipuuzi kwanini hakuzalisha fedha aliyoachiwa hebu sikia sababu zake za kipuuzi .

MATHAYO 25:24-29:

“Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unayevuna mahali usipopanda na kukusanya mahali usipotawanya mbegu. Kwa hiyo niliogopa, nikaenda, nikaificha talanta yako ardhini. Tazama, hii hapa ile iliyo mali yako.’

“Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu. Vema basi, ingekupasa kuweka fedha yangu kwa watoa riba, nirudipo, nichukue ile iliyo yangu na faida yake?


‘‘ ‘Basi mnyang'anyeni hiyo talanta mkampe yule mwenye talanta kumi.’Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo tele. Lakini kwa mtu yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.

Sababu anazozitoa ni za kipuuzi,nyuma ya sababu hizi zote ni uvivu tu ndio ulikuwa tatizo lake.Huyu mtumishi mvivu hakujua kuwa ukiweka fedha aridhini haiwezi kuota. Alipaswa kujaribu hata kuweka benki,angepata riba kuliko kuto fanya chochote.Na Yule Bwana alimwita ni mwovu na mvivu.


5. HUSUBIRI MPAKA MAZINGIRA YAWE SAHIHI NDIPO AFANYA KITU.



MITHALI 19:24

Mtu mvivu huuzamisha mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuurudisha kwenye kinywa chake!


Watu wavivu hawana msukumo na motisha ya kufanya mambo. Watasubiri mpaka mazingira yote yawe sahihi ,yawe vizuri ndipo utawaona wanashughulika .Baadhi ya watu wavivu hawana hamasa kabisa na kazi,hawana tamaa ya kufanya mambo makuu ndani yao.

Kuna watu waliozaliwa au kukulia katika mazingira ambayo ni rahisi kuwafanya kuwa wavivu.Wananunuliwa kila kitu,hawajajifunza kuzalisha chochote kwa nguvu zao,hawawezi kuchuma wao wenyewe. Wamezoea na kujifunza kusubiri mtu mmoja awape mkononi !

MITHALI 26:15 Mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye hushindwa kuurudisha tena kinywani mwake.


Ni vizuri watoto wafundishwe kazi wakiwa bado wadogo wasifanyiwe kila kitu! Wapo watoto wamekuwa hawajui hatakufua soksi zao tu! Kila kitu walikuwa wanafanyiwa.



6. HUTUMIA VIBAYA KILE ALICHONACHO.


MITHALI 12:27 Mtu mvivu haoki mawindo yake, bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.

Mtu huvivu atapanya na kufuja kile alichonacho.Mtu mvivu hawezi hata kukitunza kile alichonacho.Uvivu wake utamfanya hata kile alicho nacho kiharibike kabisa na kuchakaa .

MITHALI 24:30-31

Nilipita karibu na shamba la mtu mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.


Kuna baadhi ya vitu haviwafahi kabisa watu wavivu, hasa vile vinavyohitaji usimamizi na uangalizi wa karibu na marekebisho ya mara kwa mara. Ukiwapa hesabu ni hasara tupu. Kuna watu wanakaa na chakula mpaka kinaharibika kwaajili ya uvivu wa kukipika tu.

Kuna watu wanaacha nguo kwenye maji mpaka zinaharibika kwaajili ya uvivu wa kuzifua tu.Kuna watu wanaacha shamba lina haribika kwasababu ya uvivu wa kulipalilia kwa wakati.

MITHALI 18:9 Mtu aliye mlegevu katika kazi yake ni ndugu na yule anayeharibu.

Watu wavivu ni waharibifu wa vitu,wape kazi yako wataiharibu tu.

7. HUTAMANI MAMBO MENGI LAKINI HAWEZI KUZALISHA.

MITHALI 21:25-26 Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake, kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi. Mchana kutwa hutamani zaidi, lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.

Watu wavivu wanazao shauku na matamanio lakini hawezi kuzitimiza. Hata wakiwa na ndoto haziwezi kutimia.Wavivu wengi wanaota ndoto za mchana wakiwaza kuwa na mambo makubwa lakini hayatakamilika maishani mwao.

MITHALI 26:15 Mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye hushindwa kuurudisha tena kinywani mwake.

MITHALI 19:24

Mtu mvivu huuzamisha mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuurudisha kwenyekinywa chake!

8. HAKUBALI KUTAMBUA KWAMBA YEYE NI MVIVU

MITHALI 26:16

Mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wajibuo kwa busara.

Watu wavivu huwa wakubali kwamba wao ni wavivu,wana hekima machoni pa wenyewe.Hata mtu mvivu hapendi na anachukia akiambiwa wewe ni mvivu. Watu wavivu si waanzishaji wa mambo ,watasubiri wengine waanzishe na wao hatimaye wahamasike.Watu wavivu hatawakianza jambo huwa hawalimalizi,wana weka mambo mengi viporo.Wanaweza kuwa na mipango mingi lakini yote haikamiliki.

Watu wavivu si waanzilishaji wa mambo na hawamalizi yale wanayoanza. Wana maisha yalivugurukika yasiyo na mpangilio.Maisha ya watu wavivu hayana mpangilio,wana maisha yaliyo vurugika.



9. HUPENDA KUWA TEGEMEZI NA KULEMEA WATU WENGINE.


2 WATHESALONIKE 3:8

wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana, ili tusimlemee mtu ye yote miongoni mwenu.


Watu wavivu wanapenda vitu vya bure ,wanakwepa kugharimika. Wengi wanatabia za kuwalemea watu wengine na kugeuka mzigo.Watu watakusaidia lakini uje pia watu watakuchoka.Wako watu wana tabia ya kuomba omba vocha za simu,nauli na vitu kama hivyo mpaka watu wanawachoka.Kuna msemo unasema; “hakuna chakula cha bure,kile unachokiona ni cha bure ujue kuna mtu mwingine amekilipia gharama.”

I Wathesalonike 4:11-12

Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza, ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu ye yote.


10. HUFANYA KAZI ZAKE KWA ULEGEVU NA UZITO.
MITHALI 18:9

Mtu aliye mlegevu katika kazi yake ni ndugu na yule anayeharibu...


Mtu mvuvi hufanya kazi kwa uzito,kazi ya kuchukua muda mfupi na siku chache kwa mtu mvivu itachukua muda mrefu na siku nyingi bila sababu za msingi.Mtu mvivu ni goigoi,anajivuta sana katika kufanya shughuli zake.



Mwalimu M.A.MTITU




Wednesday, September 13, 2017

KUBADILISHWA KUPITIA MATESO



KUBADILISHWA KUPITIA MATESO 

Tunapokutana na nguvu za Mungu tukiwa katika mateso tunakuwa kama Ayubu.Maswali yetu yote kwa Mungu, malalamiko yetu yote yanayeyuka na tunaishia kuanguka mbele zake kwa hofu na kumwabudu.Tunakuwa hatuna tena cha kuzungumza mbele zake.
AYUBU 42:1-6

Ndipo Ayubu akamjibu Bwana, na kusema. Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu.

Baada ya Ayubu kumtaka sana Mungu ajitokeze na amjibu kwanini anamtesa,hatimaye katika sura ya 38-41 Mungua najitokeza kupitia Upepo wa Kisurisuri na kumjibu Ayubu kwa kumuuliza maswali mbalimbali.Hatimaye sasa katika Sura ya 42 Ayubu anasalimu amri anamwelewa Mungu na hana swali tena kuhusu kwanini anateseka.Kile kitendo cha kukutana na uwepo wa Mungu kinabadilisha,mtazamo wake unabadilika,maswali yake yanaisha na kukoma.


Ayubu atanapata uzoefu mpya na anahitimisha kwa kile alichojifunza pale Mungu alipomtokea. Mungu halimjibu Ayubu kwa mahojiano na sio kwa kujibu maswali yake.Mungu alijibu kwa kujitokeza tu kwa uwepo wake.Hilo tu lilitosha kumbadilisha Ayubu.

Nafikiri wakati mwingine tukiwa katika vipindi vya mateso kama Ayubu tunachohitaji zaidi ni uwepo wa Mungu tu ,huuo utamaliza maswali yetu yote.Na kubadilisha matazamo wetu kuhusu mateso tunayoyapitia.

Baada ya Mungu kutokea na Kuhojiana na Ayubu tunanona hata alipopata nafasi ya kuzungumza ,alizungumza kama mtu aliyebadilika kabisa na aliyenyenyekea sana.Hakuendelea tena kuwa na madai ya majibu toka kwa Mungu.Hakuendelea tena kushikiria msimamo wake na kusisitiza kuwa yeye ni mwenye haki hivyo hakusatahili hayo mateso.

Baada ya hapo Ayubu alikuwa kimya.Baada ya maneno yote katika sura za nyuma ,hakuna tena maneno yanayorekodiwa kutoka kwenye kinywa cha Ayubu. Kumwona Mungu,na kuelewa Nguvu za Mungu kulibadilisha kabisa mtazamo wa Ayubu.Aliifanya upya hofu yake ya Mungu na ilikuwa ni hofu nzuri.

Mambo Makuu Matano Yakujifunza Katika Vipindi Vya Mateso

Masomo haya ni ya muhimu,hasa kama kama utakuwa kwenye msimu wa maumivu na kuteseka.Kile Ayubu aligundua kupitia mateso yake miaka mingi iliyopita hata leo kinawapa watu nuru ya ukweli ambao bado haujapoteza nguvu yake.


1. Mungu anaweza kutenda mambo yote.

AYUBU 42;1-2

Ndipo Ayubu akamjibu Bwana, na kusema. Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote.

Ayubu alijifunza juu ya uwezo na ukuu na enzi ya Mungu.Alikiri kwamba hakika Mungu anaweza kutenda mambo yote.Yeye anatawala juu ya vyote.Hili ni somo kubwa sana la kujifunza.Baada ya kupitia katika mateso Imani ya Ayubu ili kuwa imetakaswa na imeimrika zaidi.Aliaamushwa na kuwa na ufahamu Mpya wa Kina kuhusu Mungu na uwepo na ukuu wake.Sasa imani yake imepita katika moto na amekuwa na kumjua Mungu kwa karibu zaidi.

Kumbe katika mateso tunapata nafasi ya kumjua Mungu kwa upya. Kuna kupata ufunuo mpya kupitia mateso ambao usingeweza kuupata kwa njia yeyote ile.


2. Makusudi yake Mungu hayawezi kuzuilika

AYUBU 42 : 2b Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. 

Jambo jingine ambalo Ayubu alijifunza katika mapito yake ni kuhusu makusudi ya Mungu. Aliyefahamu makusudi ya Mungu na akaukubali ukweli kwamba makusudi ya Mungu hayawezi kuzuilika. Ayubu alijifunza somo kuhusu njia za Mungu kwamba Mungu anakwenda kufanya kile anachoenda kufanya.

Mungu hutuamsha tuujue ukweli kwamba Yeye ni Mungu wa makusudi. Mungu anayo makusudi na maisha yetu na anapokusudia kufanya jambo haiwezekani kwa chochote kile kulizuia hilo kusudi lake.Wakati mwingine ni kupitia hayo mateso tunayatambua makusudi ya Mungu na kujisalimisha kwake.



3. Ufahamu wetu ni mdogo kuelewa Maarifa ya Mungu ya kuruhusu Mateso kwetu. 


Ayubu 42:3

Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. 

Baada ya kuziona njia za Mungu katika Ukuu na enzi yake Ayubu alikiri kwamba ufahamu ulikuwa ni mdogo sana kuelewa kwanini anateseka. Alitambua kwamba hata kama Mungu angemwelezea kila kitu anachofanya na kumchambulia kimoja kimoja bado asingeweza kuzielewa njia za Mungu kwani ni kuu sana kwa akili yake kuelewa. ( Isaya 55: 8-9). Alijifunza kwamba kuna wakati katika mahusiano na Mungu huitaji kujua kwanini; unahitaji kuwa mtii tu.


4. Maarifa ya Mungu ni makuu sana na ya kushangaza sana.

Ayubu 42:5

Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. 

Mahusiano ya Ayubu na Mungu yalikuja kuwa ni ya kina na ya karibu kwasababu ya yale aliyopitia.Ni kweli kuanzia mwanzo hata kabla ya kupitia mateso alikuwa ni mtumishi mcha Mungu na mwaminifu,lakini sasa anazunguza juu ya ufunuo binafsi alioupata wa kukutana na Mungu uso kwa uso. Kukutana kwake na Mungu kulifanya kila kitu katika maisha yake kubadilika.

Kupitia mateso uhusiano wetu na Mungu unakuwa ni wakaribu na halisi .Hakuna wakati tunakutana na uwepo wa Mungu kwa karibu kama wakati wa mateso. Ni katika nyakati kama hizo ni rahisi zaidi kupata ufunuo wa Kibinafsi kuhusu Mungu.

Wakati Shetani anataka kutumia maumivu yako kukufanya ukwazike na kukosana na Mungu;Mungu anataka kutumia maumivu yako kukuvuta kwake ili aweze kuleta badiliko ndani yako.Kitu kile kile ambacho Shetani anataka kuyatumia mateso kukufanya akuvute mbali na Mungu ,Mungu atatumia mateso haya hayo kufanya wewe kumjua Yeye kwa ukaribu zaidi kuliko Mwanzo.

5. Mateso hutufanya kupondeka na kujishusha mbele za Mungu.

AYUBU 42:6

Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu. 

Mara nyingi Mungu alipojifunua kwa watu katika Biblia ,huu ulikuwa ndio mwitikio wa kawaida.Ayubu alipotokea na Mungu katika mateso yake alipondeka na kujishusha mbele zake.Kuna hali kuu sana ya kujiona hastahili na mwenye upungufu. Ili hali ya Ayubu aliyokuwa ameing’an’gania ya kujiona ni mwenye haki na hastahili kuteseka ilikwisha.

Mateso yanatunyenyekeza na kutufanya tumtegemee Mungu.

Ayubu alifanya toba kwa maneno yake na mwitikio wake mbaya aliouonyesha katika kipindi chote cha kujaribiwa katika mateso.Tunamwona Ayubu Mpya ambaye amenyenyekea na kupondeka kabisa. Ambaye mbali na nje ya Mungu anatambua kwamba ana haki ya kujihesabia,anayetambua udhaifu wake, upungufu wake, kutokuwa na umuhimu na utupu wake .

Kwasababu ya kutakaswa kwa moto wa mateso Ayubu sasa ametoka akiwa anaweza kutembea katika unyenyekevu mbele za Mungu na kumtegemea Mungu katika maisha yake yote.

Watu wengine Majaribu yana washinda, lakini wengine yana waimarisha inategemea na namana gani tunashughulika nayo.

2 Wakoritho 1:8-10 

Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi. Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu, aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa; 

Mateso na dhiki zilimfundisha Paulo asijitegemee Mwenyewe bali Mungu.Mungu ataendelea kuruhusu mateso ,dhiki, taabu,adha mbalimbali kwa watu wake pale wanapoanza kuwa wanajitegemea wenyewe na kushindwa kumtumainia Yeye.Ni kupitia mateso watu huwa wanaona kwa urahisi umuhimu na uhitaji wa Mungu.


Mwalimu Meinrald Mtitu




Tuesday, August 8, 2017

ZIJUE DHORUBA ZA MAISHA



Dhoruba Ni Njia Ya Mungu Kukujaribu Na Kuithibitisha Imani Yako


Mathayo 14:25-31

Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? 

Wakati Yesu anawajia akitembea katika maji,wanafunzi hawakuweza kumtambua.Walifikiri ni pepo au kivuli chake.Wakapiga kelele kwa hofu.Lakini Yesu alikuja na ujumbe wa amani na wa nguvu.Alikuwa na ujumbe wa Amani kwao.

Dhoruba za maisha zina uwezo wa kumfunua Mwokozi kwetu katika njia ambayo hatu kuzingatia kabla.Anapokuja kwetu,akitembea katika dhoruba zetu,hutupa ujumbe ule ule wa matumaini ambao waliwapa wanafunzi usiku ule.

Walikuwa bado wapo kwenye dhoruba pale alipo waambia wachangamke.Kwa uweza wake,Mwana wa Mungu anaweza kutupa amani katikati ya dhoruba zetu. Hii ni amani anayoitaja katika Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. 

Yesu alipojitokeza,alitokea akisema juu ya utambulisho wake, ”Ndimi”. “Mimi Ndiye”.Ni kauri kama ile aliyoisema kwamba Mimi Ndimi mlango,Mimi Ndimi njia ,kweli na Uzima,Mimi Ndimi mzabibu wa kweli,Mimi Ndimi mchugnaji mwema.

Yesu anawaambia wanafunzi wake wa furahi, Mungu yupo hapo.Tukiweza kuukamata ukweli kwamba Yesu ni Ndimi Mkuu na kwamba ana nguvu zote mbingu na dunia sawa na Mathayo 28:18,tunaweza kufarahia amani katikati ya majaribu.

Yesu analitoa ujumbe wa uwezo,alitioa amri kwa wanafunzi wake wasiogope.Tukiweza kuona ukweli kwamba Yesu anatawala kila eneo la maisha yetu,na kwamba ni Mungu ,na kwamba anazo nguvu zote,basi tunaweza kufika mahali ambapo tunaweza kumtumaini kabisa kupitia dhoruba zote za maisha.

Dhoruba za maisha ni Baraka kwasababu zinamfunua Mwokozi katika namna mpya kabisa.

Mathayo 14: 28-29,

Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. 

Dhoruba zinatutakasa.Pale Petro aliposikia kwamba ni Bwana alitaka kujiunga na Yesu kutembea katika maji.Yesu alimwambia tu Petro njoo.Petro aliitii na yeye akatembea katima maji.Yesu aliitumia dhoruba kama namana ya kumsaidia Petro kukua katika imani.

Pale dhoruba za maisha zinapotupiga kama tunataweza kuushika ukweli kwamba Yesu ni Bwana wa dhoruba,na sisi pia tunaweza inuka juu ya mazingira yetu na kutembea juu ya mawimbi na pamoja na Bwana.Dhoruba zinaweza kuinua viwango vyetu vya imani katika kumtumainia Bwana.

Natambua fika kwamba kutembea kwa Petro hakukudumu kwa muda mrefu.Punde alipoondoa macho yake kwa Bwana alianza kuzama.Hata hivyo,Petro ameacha ushuhuda ambao wanafunzi wengine hawakuwa nao.Ni yeye pekee anayeweza kusema niliwahi kutembea juu ya mawimbi.

Hakika Mungu anaweza kuzitumia siku zetu ngumu kutufundisha zaidi kumhusu Yeye na kutusaidai kukua katika Bwana.Atatumia mawimbi kukufanya uwe zaidi kama yeye.Kumbuka kulikuwa na watu kumi na mbili kwenywe mtumbwi lakini ni mmoja tu anayeweza kusema alitembea katika dhoruba kama Yesu.

Dhoruba Za Maisha Zinatukumbusha Ni Nani Ambaye Anatawala.

Mathayo 14: 30-31 

Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

Petro alipotaka kutembea juu ya maji kama Yesu,Alimjaribu Bwana na akaingia katika maji.Hata hivyo pale alipotoa macho yake kwa Bwana na alipofanya hivyo alijikuta mwenywe kwenye matatizo. Lakini mara moja alikumbuka nani ambaye anatawala na akamwita Bwana na akapata masaada alio uhitaji.

Dhoruba za maisha zinatumika kutukumbusha sisi juu ya nani anayetawala.Kama Petro,kuna wakati tunaondoa macho yetu kwa Bwana wakati wa dhoruba zetu.Tunapofanya hivyo,tunajihakikishia kufeli au kushindwa.Tunahitaji kukumbuka nani ni msimamizi wa kila kitu.

Kama tutashinda na kufauli kwenye dhoruba za maisha hatustahili sifa kwamba ni kwa uwezo wetu au mafanikio yetu.Bali ni kwasababu kuna mmoja aliye mkuu kuliko sisi anaye tushika mkono. Mafanikio yetu na ushindi katika dhoruba za maisha yapo juu ya utayari wetu wa kutambua kwamba Yesu ni Bwana juu ya dhoruba.

KUZISHINDA DHORUBA KATIKA MAISHA YAKO


Pamoja na kuwa dhoruba katika maisha yetu sio nzuri, lakini bado zina tengeneza manufaa fulani katika maisha yetu.Kuna Baraka zilizojificha katika dhoruba za maisha zinazo tupiga sisi kama wana wa Mungu.Sijui ni aina gani ya dhoruba unayokabiliana ,lakini ninajua kwamba Bwana analo kusudi katika kuiruhusu dhoruba na tufani ipige katika maisha yako.


Mathayo 14:22,24

Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.

Katika kifungu hiki cha maandiko,tunaona vile wanafunzi wa Bwana wakiwa wamekwama katika dhoruba kali.Walijikuta katika dhoruba ile,kwasababu walikuwa wameamriwa na Bwana kuvuka bahari ya Galilaya.Watu hawa walikuwa katika mapenzi ya Mungu na bado,wanaonekana wana hangaika katika dhoruba. Pamoja na kujitahidi kote,hata hivyo,inaonekana hawawezi kusonga mbele,Upepo unawapiga usoni .Watu hawa 12 wana kwamba katika dhoruba na washindwa kutoka. 

Je umewahi kujikuta katika hali kama hiyo? Umewahi kujikuta umekwama kwenye moja wapo mwa dhoruba za maisha,na haijalishi kiasi gani umejitahidi kujaribu, inaonekana umeshindwa kwenda mbele? Sawa,sote tuna nyakati kama hizo! Inaonekana kama dhoruba haitaisha na hakuna jema litakalo kuja kutoka kile tunacho kikabili.Hata hivyo pamoja na kuwa dhoruba katika maisha sio nzuri,zina tengeneza faida /manufaa fulani katika maisha yetu.

Dhoruba Ni Njia Ya Mungu Ya Kukujia na Kujifunua katika Maisha Yako. 


Mathayo 14:25-

Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.


Marko 6:48-

Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.


Yesu alikuja katikati ya majanga ya upepo makali na mawambi makali wakati wanafunzi walipokuwa wanapigania kuokoa maisha yao katika dhoruba.Napata picha kwamba hawa watu walikuwa wanaogopa juu ya maisha yao.Wakati walipofikiria kwamba matumaini yote yamekwisha na wamebaki bila matumaini,Upande wa pili Yesu anakuja akitembea katika mawimbi yale yale na upepo ule mkali akiwaendea.

Lile jambo ambalo wanafunzi waliogopa yaani bahari iliyochafuka,ndilo hilo hilo ambalo Mungu alilitumia kama njia cha kujifunua mwenyewe kwao.Atafanya hivyo hivyo katika maisha yako na yangu.Yesu aliwajia usiku bahari wakati wanaogopa.Biblia inasema Yesu aliwajia kwenye zamu ya Nne.Ambayo ni kati ya saa 9 na 12 Asubuhi,ni katika masaa ya giza ya usiku,Yesu alikuja kwao akitembea juu ya maji.

Jambo lile wanafunzi waliloliogopa,bahari iliyochafuka,ndicho kitu kile ambacho Mungu alitumia kuwaendea wao.Huu ni ushuda wa ajabu!Hakuwa anawaambia kwamba dhoruba haikuwa kali,alikuwa anawaambia kwamba alikuwa ni mkuu kuliko dhoruba.Hilo bado ni neno lake kwako! Pamoja na kile unachokikabili katika maisha,kumbuka Yesu ni mkuu kuliko dhoruba unayoweza kuwa unaipitia.

Unaweza kuwa unatembea katika giza na unashanga Yesu yupo wapi.Unaweza kuwa unazikabili siku fulani za giza katika maisha yako hata sasa.Ngoja nikukumbushe kwamba Mungu wetu yupo siku zote pamoja nawe sasa na Neno lake katika Waebrani 13:5 ambapo anasema, “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.” 

Ngoja nikukumbushe kwamba hata katika saa ya giza kabisa ya maisha yako Mungu bado ni Mungu na bado anatawala maisha yako. Hata saa ya giza sana ya maisha haiwezi kukuficha wewe kutoka katika uso wa Mungu.Yeye yupo hapo hata kama huwezi kumwona.


Mungu anaweza asikuzuie kuingika katika dhoruba,lakini atakutunza katikati ya dhoruba.

Kuna nyakati tunajihisi kama tumepoteza vita vyetu na dhoruba zetu,lakini wacha ni kukumbushe kwamba kama vile kwa hakika Bwana anatawala baraka zako.Yeye pia anatawala dhoruba zako.Wakati mambo yanaoneka ni mabaya kabasi,hebu angalia kukuzunguka,Yesu yupo karibu kujionyesha!Kumbuka anaweza asikuzuie kuingika katika dhoruba,lakini atakutunza katikati ya dhoruba.

Fikiria juu ya Vijana watatu wa kiebrania, Fikiri juu ya Danieli na Nuhu.Mungu hakuwazuia yeyote kati yahawa kuuingia katika dhoruba,lakini aliwaokoa wote kutoka katika dhoruba zao.Kile alichofanya kwao,atafanya kwako.

Kama utakuwa na subira na kumngojea, Yeye,atajionyesha katika wakati sahihi.Utaona vile Bwana atavyoitumia dhoruba kujiweka wazi kwako. Yaani kitu kile kile kinachokuogopesha kitakuwa ni chombo ambacho Bwana atakitumia kujionyesha na kujidhihirisha ukuu wake katika maisha yako.

Mungu alitumia dhoruba ya mwiba katika maisha yake Mtume Paulo ili kujionyesha na kujidhihirisha katika maisha ya Paulo.

2 Wakoritho.12:7-10.

Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. 

Kile ninachojaribu kukuambia ni hiki: “ Usiogope dhoruba katika maisha! Dhoruba imesanifiwa na Bwana kama njia ya kumleta Yeye karibu kwako.Aliyazipanga na zipo kwaajili ya faida yako.”

Warumi 8:28 “ Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”

Mungu Akubariki.

Tuesday, August 1, 2017

UKUAJI WA KIROHO






UKUAJI WA MAISHA YA KIROHO


Kukua kiroho ni maendeleo ya uhusiano wako na Mungu

Agano Jipya limeweka wazi kuwa mapenzi ya Mungu kila mwamini akomae kiroho. Mungu anataka sisi tukue.Neno ya kiyunani lenye maana ya “kukua” lina maanisha “ Kuongezeka,kuwa mwenye kuzaa zaidi au kuwa mkuu”. Wengine tunaposikia kukua kiroho tunaweza kujaribiwa na kufikiri hili jambo linawahusi wa Kristo wachanga walioamini hivi karibuni.Hivyo wao haliwahusu.

Kukua kiroho ni jambo linalomhusika kila mtu aliye mwamini Kristo.Bila kujali lini alifanya hivyo na haya ni mapenzi ya Mungu kwa kila mkristo.Mungu hataki sisi tubakie katika hali ile ile kiroho mwaka hata mwaka. Anatamani kutuona tunabadilika kutoka hatua moja ya utukufu kwenda nyingi mpaka tumegeuzwa katika sura ya Kristo.


Waefeso 4:14

“Ili tusiwe tena watotowachanga, tukitupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu...lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie Kristo”.


Mungu anataka kila mwamini awe na tabia ya Kristo.Swali kubwa kwa hiyo ni: Ni kwa namna gani kukua kiroho kunatokea? Tunawezaje kukua ndani ya Kristo?






Maana 7 Za Kukua Kiroho

1. Kukua kiroho ni mchakato wa kufanyika kuwa zaidi kama Yesu Kristo.


Lengo kuu la kukua kiroho ni kuwa kama Yesu. Mpango wa Mungu kwetu sisi tangu mwanzo ni sisi tufanane na Mwanawe. Kukua kiroho ni kubadilishwa kwako kuelekea kufanana na Yesu.

2 Wakorintho 3:18

Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

Warumi 8:29

Maana wale aliowajua tangu asili wafananishwe na mfano wa ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

Tunapoweka imani zetu kwa Yesu,Roho Mtakatifu huanza machakato wa kutufanya kuwa kama Yeye,akitugeuza katika mfano wake.Kukua kiroho penginekunaelezwa vema zaidi katika 2 Peter 1:3-8, ambapo tunaelezwa kwamba kwa Nguvu za Mungu tunacho kila kitu tunachohitaji kuishi maisha ya utauwa ambalo ndio lengo la kukua kwetu kiroho.

Kila tunachohitaji kinatoka kupitia maarifa yetu ya Yeye,ambao ndio ufunguo wa kupata kila tunacho hitaji.Maarifa ya kumjua yanakuja kutoka kwenye Neno tulilopewa kwaajili ya kujengewa na kukua kwetu.


2. Kukua kiroho ni kuongezeka kwa tunda la Roho katika maisha yetu.


Kukua kiroho ni upanuzi wa kutegemea kwako katika kuenenda katika Roho.Kukua kiroho kunaainishwa na Tunda la Roho linavyo ongezeka na kuwa dhahiri katika maisha yetu.

Katika Wagalatia 5:19-23 kuona orodha mbili hapo.Mstari wa 19-21 kuna orodha ya “matendo ya mwili”.Haya ni mambo ambayo yalitambulisha maisha yetu kabla hatujaja kwa Kristo kwa Wokovu. Matendo ya mwili ni mambo ambayo tunaya ungamana na kuyatubu na kwa msaada wa Mungu tunayashinda.

Kadiri tunavyopata uzoefu wa kukua kiroho,ndivyo matendo ya mwili machache zaidi yatajionyesha katika maisha yetu.Kwa lugha nyingine ni kwamba kadiri tunavyi kua kiroho ndiyo matendo ya mwili yanavyi zidi kupotea katika maisha yetu.

Orodha ya pili ni ya Tunda la Roho hii ni mstari wa 22-23.Haya ni matendo ambayo yanapaswa kuwa ni tabia katika maisha yetu baada ya kuwa tunapata wokovu katika Kristo.Kadiri tunavyozidi kukua ndivyo nayo yanavyozikuwa dhahiri katika maisha yetu. 

3.Kukua kiroho ni kazi ya Mungu inayoendelea katika maisha ya muumini baada ya wokovu.

Kukua kiroho ni mwendelezo wa kilichofanyika katika wokovu, wakati maisha mapya yanapotolewa kwa muumini na kuwekwa ndani ya muumini.Kuna pande mbalimbali za ukuaji wetu. Roho Mtakatifu anatuhuisha ili kwamba tuweze kubadilishwa katika sura ya Mungu. Lakini mabadiliko haya ni hatua inayoendelea, na hatua hii inasonga mbele kwa ushirikiano wa Mungu na Mkristo.

Tumeambiwa katika


Wafilipi 2:12-13,

“utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka, kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yangu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.”



Hapa tunaona ushirika ambao ni lazima tufanye na Mungu. Hatuwezi kukaa tu bila kufanya kitu na kufikiri kwamba Mungu peke ataweka ndani yetu kumfanana kwetu. Lazima na sisi tujihusishe vilevile. Ni lazima “tufanye kazi.” Lakini kazi hii siyo ya kutufanya tukubalike na Mungu; isipokuwa ni kuonyesha kuelewa kwetu na kuonyesha shukurani ya msamaha wa dhambi zetu kupitia damu ya Yesu Kristo na kurithiwa kama watoto wa Mungu.


 4. Kukua kiroho ni hali ya mabadiliko ya wokovu kuchukua nafasi ndani yako.

Kukua kiroho ni hatua ya kuuvua utu wa kale na kuuvaa utu mpya.Wengine wanatazama kukua kiroho kama hatua ya kubadilisha utu wa kale wa dhambi kwa utu upya unaotokana na Kristo. Kadiri mtu wa kale anapokufa, mtu mpya anatokea. Wakati hii inapotokea, mtu anakua kiroho.

Pale mabadiliko ya wokovu yanapochukua nafasi ndani ya mwamini,kukkua kiroho huanza.Roho Mtakatifu hufanya makao ndani yetu.(Yohana 14:16-17). Sisi tu viumbe vipya ndani ya Kristo. Utu wetu wa kale wa dhambi unaanza kuacha njia kwaaji ya utu mpya ,Wenye asili ya Kristo.( 2 Kor.5:17, Warumi 6-7).Kukua kiroho ni mchakato mrefu wa maisha yote ambao unategeme na vile tunajifunza na kulitendea kazi Neno la Mungu na kutembea kwetu katika Roho.( 2 Timothy 3:16-17).


5. Kukua kiroho ni kukua katika ufahamu wa kumjua Mungu
Kumjua Mungu ndiyo kusudi na maana ya uzima wa milele. Kisa hasa cha kutaka maisha ya kikristo inatakiwa iwe kumjua Mungu katika kweli. Kwa hiyo, tunapoendelea kukua kumjua yeye katika ukuu wake wote, tunakua kuwa kama yeye.
Nafasi ya kwanza ya utaratibu wa ukuaji inahusisha kukua katika mwanga wa Mungu. Katika Yohana 17:3 Yesu anasema, “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo aliyetumwa.”

Kadiri tunavyokua katika kumjua Mungu, ndivyo tunavyobadilishwa zaidi na zaidi kuwa katika mfano wake.Ufunguo wa kumjua Mungu ni kuelewa tabia yake ya utakatifu. Tunajifunza kuhisi kama mtume Paulo alivyosema, “Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu” (Wafilipi 3:8a). Hii ni sehemu ya hatua ya utakaso.

Tunapokuwa tunakua katika mwanga wa Mungu katika ukamilifu wake wote, tunakua na kujitambua wenyewe pia. Kipekee, tunafikia kujua hali yetu ya dhambi tofauti na tabia kamilifu ya Mungu. Kadiri tunavyomsogelea karibu Mungu, ndivyo tunavyojiona kuwa mbali naye. Kadiri tunavyomjua alivyo mtukufu kweli, ndivyo kadiri dhambi zetu zinavyodhihirika mbaya zaidi kwetu.


Yeremia 9:23-24

“Bwana asema hivi, mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake, bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifamu mimi na kunijua ya kwamba mimi ni Bwana, nitendaye wema na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo , asema Bwana”


6. Kukua kiroho ni mchakato wa kufanyika kuwa Mwanafunzi wa Yesu.

Biblia inatufundisha kwamba Waamini waliokomaa ndio wanaoitwa wanafunzi.Hili ni Neno ambalo Biblia linatumia kwa waamini waliokomaa tu.Mtu hawezi kuwa mwanafunzi bila ya kuwa chini ya nidhamu.Maneno mwanafunzi na nidhamu yana kwenda pamoja .Disciple – discipline.kadiri ninavyo kuwa nimetiwa nidhamu ndivyo nitavyotumiwa zaidi na Mungu.

Alama ya uanafunzi ni kubeba Msalaba.Mungu anatutaka sisi kubeba Misalaba yetu.Luke 14:27, Luke 9:23.Msalaba huo unabebwa kila siku na kumfuata kila siku.Kubeba msalaba kuna husisha kufanya chochote kila ambacho kitamfanya Kristo kuwa na nafasi ya kwanza katika maisha yangu.


7. Kukua kiroho ni kukua katika Utakatifu wake.


Baada ya kumjua Kristo kama mwokozi, tunatakiwa tuendelee kukua katika mwanga wetu wa utakatifu wa Mungu na katika utambuzi wa hali zetu za dhambi. Hii inaweza kuwa uzoefu wa kuhofisha.
Kumjua Mungu na Utakatifu wake ni kukaribisha kujiweka wazi wenyewe, na huu ni uzoefu wa kutisha kwa hao wanaopenda kuficha makosa yao na mapungufu. Kwa jinsi hiyo, kwa mkristo anayekua, pengo linaonyesha hitaji la kuendelea kumhitaji Kristo na ukuu wa yale aliyofanya msalabani

Kadiri tunavyomjua Mungu ndivyo kadiri tunavyojiona kutofaa mbele zake. Mwanga huu unapokua,tunaona maana ya msamaha wetu na upatanisho wetu kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.

Tunapoufahamu ukuu wa Mungu, (kama Isaya alivyofanya alipoona utukufu wa Mungu hekaluni, au kama taifa la Israeli walivyofanya walipokutana na Mungu katika mlima Sinai). Tunagundua utukufu wa kweli wa mwokozi. Damu yake inaosha wenye dhambi na kuzisafisha na kutuvalisha mavazi meupe ili kwamba tuweze kumsogelea Mungu huyu wa utukufu.


Pastor Meinrald Mtitu.

Friday, July 28, 2017

JINSI YA KUISHI KAMA NDEGE WA ANGANI


JINSI YA KUISHI KAMA NDEGE  WA ANGANI


“Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

Ndege wa angani hawalimi, hawavuni ila wanakula na maisha yao yanasonga mbele. Na wewe unaweza kusema kwamba kumbe hakuna haja kubwa ya kuhangaika na kuweka juhudi kwa sababu hata nisipofanya hivyo bado nitakula na kuishi. Inasikitisha kuona kwamba dhani hii ya kuishi kama ndege ipo bado katika fikra za baadhi ya watu makanisani.


Ndege wa angani hawalimi, hawavuni ila wanakula na maisha yao yanasonga mbele. Je, nasisi hatuna haja ya kuhanganika kwasababu bado tutakula kula na kuishi tu kwa neema za Mungu?

Katika Mathayo 6:26 tunasoma hivi,

“Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?”

Kufikiria kwamba kifungu hiki kinatupa uhuru wa kukaa bure na kusubiri maisha yaendee yenyewe kwa neema ya Mungu hivyo kutoweka juhudi kubwa kwenye kile tunachofanya ni makosa makubwa.Ukitafsiri hivyo basi wewe umepotoka kwa sababu kuna mambo mengi sana ambayo hao ndege huwa wanayafanya ambayo unatakiwa kuyafanya na huyafanyi.

MAMBO USIYO YAJUA KUHUSU MAISHA YA  NDEGE



Ndege ni viumbe hai wenzetu ambao tumekuwa tunawaona ni viumbe wa kawaida tu lakini wana somo kubwa la kutufundisha. Japo viumbe hawa hawawezi kuongea na sisi moja kwa moja, ila vitendo vyao vinaonesha wazi wazi na hivyo mtu unaweza kujifunza na kuboresha maisha yako sana.

Ingawa Andiko hilo linaeleza upande mmoja tu wa ndege kula bila kufanya kazi na kulishwa na Baba wa Mbingu lakini kuna upande wa pili ambao umefichika. Ndege hao mpaka wapate chakula ambacho Baba wa Mbinguni anawapa kuna mambo mengi sana wanayakabiliana nayo.Hivyo na wewe unayetaka kukaa tu na kulishwa kama ndege lazima uwe tayari kuyapitia ili ufanane nao.

Mambo matano(5) ya kujifunza toka kwa ndege Ambayo hufanya kabla ya                                    kulishwa chakula :

Kwa kuangalia huu mfano wa ndege ambao hawalimi ila wanakula tutajifunza na kuona ni jinsi gani ndege ni waerevu kuliko wewe. Haya utayojifunza yatakusukuma zaidi na kukufanya uamue kuyachukua maisha yako kwenye mikono yako na kuwajibika nayo.


1. Ndege ni watafutaji chakula chao hakitokei kwenye kiota chao bali kinatafutwa:

Ni kweli ndege halimi, wala havuni na kukusanya ghalani lakini pia chakula chao hakitokei pale pale kwenye kiota chao. Ni lazima watoke wakatafute na hata kwenye kutafuta hawakutani nacho kirahisi tu. Wanapitia mazingira magumu sana, wengine wanakoswa koswa kuliwa na Wanyama wengine na ndege wanaokula ndege, wengine wanakoswa koswa kuwindwa lakini wanachukua hatari yote hiyo ili wapate chakula.

Sasa wewe unayetaka kuishi kama ndege lakini haupo tayari kuchukua hatari yoyote ili kuboresha maisha yako basi umepotoka. Unajaribu kufanya kazi fulani kidogo na ukiona hatari unakimbia haraka sana na kukata tamaa. Ndege haishi hivyo.Hapa ni sawa na ndege akoswe na mwindaji siku moja na aseme sitaenda tena kutafuta chakula, nakaa hapa kwenye kiota changu tu. Jifunze somo hili;



Kama unataka mabadiliko kwenye maisha yako ondoka hapo kwenye kiota chako leo. Kama utaendelea kungangania hicho kiota jua hakuna kitakacho badilika.Kiota chako ni hali yoyote ambayo imekuridhisha kwa sasa. Hali ambayo inakufanya uogope kuchukua hatua kwa kudhani ni hatari mno. Maisha yote ni hatari hivyo usiogope kufanya jambo ambalo ni muhimu kwako kwa sababu unaogopa kushindwa.


2. Ndege wana amka mapema asubuhi mwanga ukishatoka na kuanza kutafuta chakula.


Saa kumi na moja na nusu asubuhi tayari utawasikia ndege wanalia huko nje. Hivi umewahi kukuta ndege amelala mpaka saa mbili? Sawa, hata wewe huwa hulali mpaka saa mbili, labda nikuulize hivi tena. Umewahi kukuta ndege amelala mpaka saa mbili kwa sababu siku hiyo ni siku ya jumapili? Au siku ya sikukuu?

Haijalishi ni siku gani kwenye dunia yao, mwanga ukishaonekana tu ndege nao wameamka na wanaendelea na mchakato wao wa kuboresha maisha yako. Sijui kama kuna ndege ambaye huwa anajishauri mara mbili mbili kwamba aamke au asiamke. Na sijui kama kuna ndege ambaye ana alarm anayoweza kuizima na kulala kidogo, dakika tano tu ila anakuja kustuka nusu saa baadae, kama unavyofanya wewe mara kwa mara.

Unakumbuka usemi kwamba ndege anayewahi kuamka ndiye anayepata wadudu wazuri wa kula. Nafikiri hilo halina ubishi, kama kuna mdudu alichelewa kujificha basi ndege anampata kwa urahisi kabisa anapokuwa ameamka mapema. Jifunze somo hili kwa ndege,


Anza siku yako kwa kuamka mapema kila siku, haijalishi ni siku gani. Anza siku yako mapema.
Kuwa na utaratibu wa kuamka mapema kila siku na tumia muda huo kutafakari maisha yako, kupangilia siku yako, kujisomea na hata kufanya kazi zako, kama kazi zako zinawezekana kufanya kwenye muda huo.

Usiache hata siku moja kuamka mapema na usiamke halafu ukaanza kujishauri. Kama unatumia alarm kuamka ikishaita tu, ruka kutoka kitandani na unapoanza kupata mawazo kwamba urudi kulala, jiulize je ndege angefanya hivyo? Kama jibu ni hapana ondoka kitandani na kawahi wadudu wazuri.Wadudu kwako ni zile shughuli muhimu kwako.


3. Hakuna ndege anaye lalamika kwaajili ya hali yake

Sijawahi kuona ndege wa kitajiri, Sasa swali ni je umewahi kumuona ndege wa kitajiri?Yaani ndege ambaye wazazi wake ni matajiri? Na je juhudi zake zinatofautiana na ndege ambaye ni wa kimasikini?


Nafikiri tunakubaliana kwamba hakuna ndege anayekaa chini na kusikitika kwamba leo siwezi kwenda kutafuta chakula kwa sababu wazazi wangu hawajanisaidia. Au ndege analalamika kwamba wazazi wake hawakufanya kitu fulani ndio maana maisha yake sio mazuri. Au ndege anawaambia wazazi wake wampe urithi! Jifunze jambo hili;

Ni marufuku kutoa sababu ya kijinga kama hiyo eti maisha yako sio bora kwa sababu wazazi wako hawakukusomesha, au hawajakupa mali, au ni masikini.Kama umeweza kuwa na akili ya kufikiria hiki, jua kwamba chochote unachotaka kipo kwenye mikono yako.


4. Ndege hawana malalamiko yao kwa serikali.
Labda ndege wana serikali yao, na wana vyama? mimi sijui lakini ninachoweza kusema ni kwamba sijawahi kuona ndege ameacha kwenda kutafuta riziki yake kwa sababu chama chake au serikali imewaahidi maisha bora. Sijawahi kuona ndege ameacha kuweka juhudi kwenye kutafuta riziki yake na kutumia muda huo kulalamika kwamba serikali yao imefanya hiki, mara imefanya kile na kuitumia kama sababu ya kutokupata riziki.

Tunahitaji serikali nzuri lakini hilo sio jawabu la matatizo ya maisha yako.Kama unaamini serikali ndio itakuletea wewe maisha bora umepotoshwa na ukakubali kupotoka.Kama unaamini serikali ndio jibu la matatizo yako umepotoka pia. Lakini mbona niliahidiwa maisha bora na kuhakikishiwa hivyo? Sawa uliahidiwa, je umeyaona maisha hayo bora/ Maisha bora yapo kwenye mikono yako.

Usidanganyike kwamba kuna serikali itakuja kukuletea wewe ugali ukiwa umekaa unabishana au kusifia kwamba serikali ni nzuri. Hivi unajua serikali inakutegemea wewe ndio iende. Yaani wewe usipofanya kazi hakuna mshahara wa kumlipa Raisi.Tunahitaji serikali nzuri lakini hilo sio jawabu la matatizo ya maisha yako.


5. Ndege ni wajasiriamali.

Sijui kama kuna ndege mmoja ambaye ameajiri ndege wengine au kuna ndege ambao wameajiriwa na matumaini yao yote wameweka kwa yule ndege aliyewaajiri.Ndege wanajua juhudi zao ndio zitafanya maisha yao yaendelee kuwepo. Kuna Somo kubwa la kujifunza hapa;

Ajira ni sehemu ndogo sana ya mafanikio ya maisha yako. Unahitaji kuweka juhudi nyingi binafsi ili kuweza kufanikiwa kwenye maisha yako. Kama unafanya kile tu ambacho umeajiriwa kufanya na wakati mwingine unafanya kwa kiwango cha chini sana, umekwishapotea.


Nimetumia mfano huu wa ndege ili tuweze kujifunza mambo haya matano muhimu sana kwenye maisha yako. Ndio ndege ni kiumbe mdogo sana, huwezi kumlinganisha na sisi binadamu, sawa kabisa, je kwa hayo anayofanya hajakuzidi maarifa? Hebu anza kuyafanyia kazi hayo mara moja na yafanyie kazi kila siku kama wanavyofanya ndege halafu uone kama maisha yako yataendelea kuwa kama yalivyo sasa.

Pastor Mtitu.

KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI

Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea...