Sunday, June 25, 2017

MWENYE HAKI KAMA MTENDE

M
aisha yetu ya kiroho ni jambo la kuwekewa uzito mkubwa kuliko jambo jingine lolote.Tunapaswa kuyajali maisha yetu ya kiroho zaidi ya mambo mengine maana hapo ndipo uhusiano wetu na Mungu ulipo na ndipo maana na makusudi ya maisha ilipo.

Mungu  katika Neno lake katika Zaburi 92:12-14 anayafananisha maisha ya Mwenye haki na mti wa mtende. Kama vile mtende unavyostawi na kuchanua wakati wote na kuzaa matunda ndiyo  maisha yetu ya kiroho yanavyotarajiwa yawe  na ustawi na mafanikio, afya na ubora.

Kuna hazina kubwa na  utajiri na  katika  kila mstari ulio katika Biblia ikiwa utachukua muda kutafakari na kumruhusu Roho Mtakatifu akuangazie.

Unaweza kujiuliza maswali kama mimi nilivyojiuliza wakati naitafakari mistari hiyo.Kwanini Mungu anamfananisha mwenye haki na Mti wa mtende? Kuna nini cha tofauti au cha kipekee sana katika  mti wa  Mtende ambacho kinalingana na kufananishwa na mtu mwenye haki? Ni kwa njinsi gani mti wa mtende una kua na  unastawi? Na maswali mengi kama hayo.

Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengine mengi  ilinilazimu kuanza kufanya tafakari ya kina ambayo nilifanya kwa  kipindi kirefu juu ya mistari hiyo



ZABURI 92:12a
                                                                                                                                                                                                                          “Mwenye haki atasitawi kama mtende”

“Mungu ametumia picha ya  mti wa Mtende  kumfananisha  na mtu mwenye haki”

    N
eno  “mwenye haki” sio neno linalosikika vizuri masikioni mwa baadhi ya  watu.Kama mtu atakuita  “mwenye haki” unaweza usijisikie vizuri  na kushituka.Pengine usingejali sana  kama ungeitwa “mtu mwema”, “Mtu mzuri” na majina mengine kama hayo lakini sio kutiwa  “mwenye haki”. Kwa namana fulani jina hili linashitua.

Sababu kubwa ni kwamba neno  “mwenye  haki” linatukumbusha juu ya “kujihesabia haki.” Mtu mwenye kujihesabia haki ni yule ambaye anafikiri  anaweza kujifanya mwenyewe kuwa mwenyewe haki kwa matendo yake fulani mazuri na mema anayotenda.Mara nyingi anajifikiria na kujiona yeye ni bora kuliko wengine wote. Ni kama vile mafarisayo walivyokuwa.

KWELI YA KIROHO;
Kama ambavyo mtende uliopandwa nyumbani Bwana na kustawi  ndivyo yalivyo maisha ya mtu ambaye ana Ana mahusiano na Mungu na amehesabiwa haki na kufanywa mwenye haki wake.

Maana ya  kuwa Mtu Mwenye haki

Biblia inapotumia neno mwenye haki haina maana hiyo.Hivyo hatupaswi kulikwepa neno hili au kujisikia vibaya linapoitwa kwetu, Mungu mwenye amelitumia  kwa watu wake.Katika Agano la kale neno hili limetumika sana kuwaelezea watu wanao mcha Mungu.

Mtu yule ambaye amedhamiria moyoni mwake kumcha Mungu wa kweli, huyo ndiye anaitwa mwenye haki.

Kuwa  mtu mwenye haki katika muktadha wa kibiblia  ni kuwa kinyume cha mtu mwovu.Na unaweza kuwa mwenye haki bila ya kujihesabia haki.Kuwa mwenye haki ni sawa na kuwa mtu mtauwa.Ni kitu ambacho sisi   sote tunapaswa kutamana kuwa. Mtu yule ambaye amedhamiria moyoni mwake kumcha Mungu wa kweli, huyo ndiye anaitwa mwenye haki.

Mungu ndiye mwenye kutuhesabia haki na kutuita wenye haki.Watu waliomcha Mungu wakati wote walijua kuwa hawajawa wenye haki kwa  juhudi zao wenyewe.Walijua kuwa haki yao inategemea kabisa Neema ya Mungu.

Mungu anatupa picha ya mwenye haki na ahadi alizonazo mtu mwenye haki  ambaye amemfananisha na mti wa mtende na mwerezi.Katika somo hili tuna angalia zaidi picha ya mwenye haki kama mti wa mtende.

Kitabu cha Mithali na Zaburi ni vitabu ambavyo vinaonyesha faida za kuwa mwenye haki ,na mara nyingi vimefanya ulinganifu baina ya mwenye haki na asiye haki au mwovu.

Katika Zaburi 92 kabla ya Mungu kutupa picha ya Mtu mwenye haki  yupo vipi ana anza kwanza  na kutupa picha ya mtu asiye haki vile alivyo.
Zaburi 92:7
Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;


MUNGU AKUBARIKI.

No comments:

Post a Comment

KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI

Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea...