Tuesday, June 27, 2017

KUPANDWA KAMA MTENDE


KUPANDWA KAMA MTENDE

“Wenye haki wanafananishwa na mitende iliyopandwa  katika  uwanja wa nyumba ya Bwana”

Zaburi 92:13
Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.


    M
ti huu katika Zaburi hii sio wakaida kwasabu ya mahali ulipo.Umepandaka uwanja katika Nyumba ya Bwana.Hekalu katika Yerusalemu  lilikuwa ni Nyumba ya Mungu ambapo aliishi kati ya watu wake.Na kulikuwa na eneo la uwanja ambako mti ulipandwa pale.

KWELI YA KIROHO:

Kama wewe ni mwenye haki Zaburi inatuambia kwamba  wewe ni kama  mfano wa mti Wenye  nguvu na afya uliopandwa katika nyua au uwanja wa nyumba  ya Mungu.

Kweli Tano  (5 )kuhusu  kupandwa nyumbani  Mwa Bwana:
1.      Kupandwa Nyumbani mwa Bwana kunatufanya tuwe wenye haki.

Neno kupandwa lililotumika hapo, kiebrania ni Shathal  ambalo kwa  lugha ya kiingereza ni “to be transplanted “,yaani kuhamishwa na kupandwa mahali pengine. Hivyo ni kusema wenye haki wamehamishwa kutoka mahali pengine na kuja kupandwa kwenye uwanja uliopo katika nyumba ya Bwana.

Katika hali ya kawaida mti hauwezi kupandwa katika nyumba ya Bwana,kama umepanda katika uwanja nje ya jengo basi kuna mtu ameuhamishia hapo toka ulipo kuwa na kuupanda .
Hii ni picha ya kutuonyesha vile ambavyo kuwa mwenye haki si kitu kinafanyika kwa nguvu zako mwenyewe,si wewe unayejifanya kuwa mwenye haki,sio juhudi zako,ni Mtu mwingine anaye kuhamisha na kupanda upya na kukufanya mwenye haki.

Katika hali ya kawaida mti haumei au kuota ,katika nyumba Bwana.Hata sisi hatukuanzia nyumbani mwa BWANA ,tulihamishwa kutoka mahali kwingine na kupandwa, kwa kwaida  na kwa asili si wanyumbani mwa Bwana. Huwezi kuwa mwenye haki  mpaka uhamishwe na kupandwa huko.
2.      Kupandwa nyumbani mwa Bwana kunatufanya kuwa hai kiroho
Mti wa mtende unaotaja kwenye zaburi ni mti ulio hai,unaishi. Wenye haki kwa mfano wa mtende wako hai kiroho Ni wenye haki peeke yao walio hai kiroho.Wasio haki hawako hai kiroho,ni wafu.
Kama ambavyo huwezi kupandikiza mti usio na uhai,unapandikiza mti wenye uhai ,kwa namana hiyo hiyo mwenye haki ana uhai ndani yake,Sio tu ni hai kimwili bali ni hai kiroho.Mungu ndiye chanzo cha uzima wake.( Waefeso 2:5)
3.      Kupanda nyumbani mwa Bwana kunatufanya tuwe  na mahusiano ya karibu na Mungu
Kila mtu uliokua katika uwanja wa hekalu lazima uwe umeleta kutoka mahali pengine na kupandikizwa.Na hauwezi kujipandikiza wenyewe n lazima mtu mwingie aupandikize. Kwa jinsi hiyo hiyo Mungu anatufanya wenye haki.Mungu si tu ametupa uzima na kutufanya hai kiroho lakini pia ametuleta karibu naye katika mahusiano.
Mungu ametutoa mbali na kutuleta kutupanda katika nyumba yake,mahali ambapo yeye yupo.Hii ni picha ya mahusiano ya karibu ya Mungu baada ya kufanywa kuwa wenye haki wake ,Mungu amtuleta karibu naye kiroho.(Waefeso 2:13, Wakolosai 1:13)

4.      Kupandwa nyumbani mwa Bwana kunatufanya tuwe katika mahali pa heshima na utukufu.
Kuna maeneo ya heshima ambako mti ukipandwa hapo ni sehemu maalumu sana.Si kila mahali pana weza kuupa mti hadhi.Kupandwa kwa mti wa mtende nyumbani mwa Bwana ,katika eneo la hekalu ni heshima kubwa.Hekaluni ni mahali pa heshima na utukufu.Si mahali kama mahali pengine pa kawaida.Hekaluni palikuwa ni Nyumba ya Mungu duniani,palikuwa ni mahali uwepo wa Mungu hapa duniani katikati ya watu wake wa agano.
Kitendo cha kuwa mwenye haki ni kitendo cha kupewa heshima kubwa,ni kama mtende uliopanda hekaluni mahali pa heshima kubwa.Kuwa mwenye haki ni kupatanishwa na Mungu kupitia Yesu Kristo.Ni kuingizwa na kuasiliwa katika familia ya Mungu.Tuna mahali pa heshima kama mtende uliopandwa kwenye nyua za Bwana.
5.      Kupandwa nyumbani mwa Bwana ni kuwa katika mahali pa Ulinzi na usalama.
Mti uliopandikizwa katika nyua ,viwanja vya hekalu una usalama na ulinzi mkubwa.Mti huu utalindwa dhidi ya kuwa wazi na kupigwa na upepo makali.Mti huu utalindwa na kukatwa na watu kwaajili ya kuutumia kama mbao au kuni.Nyuani mwa Hekalu ndipo mahali salama kabisa Ulimwenguni kwa mti kuwa.
Hii ni picha ya kupendeza ya usalama na ulinzi wa Mwenye haki wa Mungu.Ukweli huu ni kwetu pia,kila ambaye ni wa Mungu ndani ya Kristo yupo salama. Unapokuwa ni wa Mungu,macho yake yanakutaza siku zote.Upendo wake unakuzunguka.Na unakuwa salama dhidi ya wale wanaotaka kukudhuru,Hawawezi kukudhuru.
Katika Yohana 10 Yesu anazungumza juu ya usalama tuliona nao kwake.Paulo anzungumza hakuna kitu cha kututenganisha na upendo wa Kristo.

Mchungaji na Mwalimu,M.A.Mtitu
Ligh of Hope Teaching Ministries

No comments:

Post a Comment

KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI

Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea...