KUWA
MSHINDI KAMA MTENDE
ZABURI 92:12-13
Mwenye haki atasitawi kama mtende, …Waliopandwa katika nyumba ya
Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.
M
|
tende ni mti unaobeba alama ya mafanikio na ushindi.
Kwa miaka mingi matawi yake yametumika kuonyesha alama ya ushindi furaha na
Amani.Mara
nyingi katika Neno la Mungu kila mahali matawi ya mitende yalipo tumika
yalihusianishwa na ushindi.
Mfano Kwenye hekalu la Sulemani Tunaona
mitende ilikuwa ni moja ya michoro iliyokuwepo kwenye hekalu la Sulemani
ikiashiria ushindi.Matawi ya Mitende tunaona yakitumika kumshangilia na
kumwimbia Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu.
YOHANA 12:12-13
Siku iliyofuata umati mkubwa
uolikuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. Basi
wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti
wakisema, “Hosana! Amebarikiwa Yeye ajaye kwa Jina la Bwana! Amebarikiwa Mfalme
wa Israeli!’’
Katika
Kitabu cha UFUNUO 7:9-10 tunaiyona
mitende ikitajwa na ikieleza vile Watakatifu walio vaa mavazi meupe wakiimba kwa ushindi
mkuu wakiwa wameshika matawi ya mitendi mikononi mwao wakiashiria Ushindi.
“Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana
ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na
lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,
wamevikwa mavazi meupe, wana matawi
ya mitende mikononi mwao;”
KWELI YA KIROHO:
Mungu
anawafananisha wenye haki na miti ya mitende kwasababu anawataka wawe na maisha
ya Ushindi.Wenye haki ni washindi ndani ya Kristo.Ndani ya Kristo Wanashinda na
zaidi ya kushinda.
Biblia inatumia majina
mengi kuwaelezea wale walio ingia katika maisha
ya uhusiano binafsi na Bwana Yesu Kristo,moja ya majina hayo wanaitwa ni
Washindi.Hiki ni cheo ambacho Yohana anakitumia katika nyaraka zake.
I Yohana 5:4
“Kwa
maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kuushinda
kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu”
Mtume Paulo naye
anawaeleza wale walio mwamini Kristo kama ni watu walio washindi na wenye
ushindi katika mambo yote.
WARUMI
8:37
Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na
zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda
Mshindi Ni Nani ?
Mshindi kwa kiingereza overcomer katika maana ya kawaida ya lugha ya kiyunani “nikao” ni victor, pia
tunapata neno nike. Ambalo wayunani walilitumia kama jina la mungu mke
wa Ushindi. Katika Imani zao waliamini ushindi unapatikana kwa miungu tu na sio
wanadamu,miungu tu ndio ilikuwa washindi na walikuwa hawashindwi.
“Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda
ulimwengu. Huku ndiko kuushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.-
Mtume Yohana,” 100 A.
Sisi tu washindi wa
wokovu,ni wale tu waliozaliwa na Mungu ndio washindi wa kweli.Ushindi wetu ni
kwasababu tu tupo ndani ya Kristo aliye mshindi.Yesu alitumia neno hili nikao katika Yohana 16:33
pale aliposema “kwa maana Mimi nimeushinda
ulimwengu.’’ Ni neno Mshindi.Yesu alikuwa anasema
kwamba ameushinda mfumo wa Shetani.
Ukweli kuhusu maisha ya Mkristo ni kwamba yupo ndani
ya Kristo,hawezi kutenganishwa katika Muungano wake na Kristo mwenyewe hivyo yu
mshiriki wa asili ya uungu.Mkristo anashiriki kila kitu alicho nacho Kristo,
Hii ni pamoja na urithi,haki,mauti,uzima na Roho.Kwa vile Kristo ni mshindi na Mwamini pia ni Mshindi.Wale walio zaliwa
na Mungu ndio washindi wa kweli.